DKT. CHANA ATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MASLAHI YA TAIFA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana
kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya RITA, 22
Desemba, 2023 Jijini Arusha.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana
akihutubia wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya RITA,
22 Desemba, 2023 Jijini Arusha.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa watumishi wa umma kufanya kazi kwa
weledi na uadilifu kwa kuzingata maslahi mapana ya Serikali na Taifa kwa
ujumla.
Dkt. Chana ameyasema hayo wakati
akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi ya RITA tarehe 22 Desemba,
2023 linalofanyika Jijini Arusha. Baraza hilo linafanyika ikiwa ni utekelezaji
wa Sheria ya ajira na Mahusiano kazini.
Amesema, “huduma ya usajili wa
matukio muhimu ya binadamu na Takwimu mnazotoa ni huduma zinazowagusa wananchi
moja kwa moja. Hivyo, mkiwa wafanyakazi mlioaminiwa na Serikali ya Tanzania
endeleeni kutekeleza majukumu yenu kwa weledi na uadilifu kwa kuzingata maslahi
mapana ya Serikali na Taifa kwa ujumla.”
Amezitaja huduma zinazotolewa na
RITA kuwa ni pamoja na usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Watoto wa
kuasili, Usimamizi wa mirathi, Usajili wa Bodi za Wadhamini, Kuandika na
kuhifadhi wosia miongoni mwa zingine.
Dkt. Chana amemshukuru Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa
falsafa ya R 4 hususan kwenye maboresho ya huduma zinazotolewa na Wakala wa
RITA huku akiuagiza uongozi wa RITA kushughulikia changamoto mbalimbali za
watumishi. “shughulikieni changamoto za wafanyakazi waweze kufanya kazi kwa
furaha na ufanisi kwa kuwa mtumishi akiwa na furaha katika kazi ni wazi utendaji
wake utakuwa wenye tija.”
Aidha, Dkt. Chana amehimiza umoja
miongoni mwa wafanyakazi wa ofisi ya RITA akiwataka wajenge Utumishi wa Umma
wenye kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utumishi, kupinga rushwa na kuheshimu
sheria.
Comments
Post a Comment