MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA YAANZA VIWANJA VYA NYERERE DODOMA

 






Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe. Dkt. Juliana Masabo akisaini kitabu cha mahudhurio kwenye Banda la Wizara kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria, tarehe 24 Januari, 2024 viwanja vya Nyerere Square

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Madhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania kila mwaka yameanza leo tarehe 24 Januari, 2024 kwenye viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma ambapo Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki.

Maadhimisho hayo ya siku tisa yaliyobeba kauli mbiu ”Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai” yatazinduliwa rasmi tarehe 27 Januari, 2024 na kufungwa rasmi tarehe 1 Februari, 2024. Wakati wote wa maadhimisho hayo Wizara itakuwa inatoa elimu ya sheria na huduma ya msaada wa kisheria.

 

 




Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA