TUKO VIZURI KWENYE SUALA LA AMANI – DKT. CHANA
Wakili wa Serikali Mkuu
Bw. Emmanuel Mbega akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi
Dkt. Pindi Chana alipotembelea banda la Wizara, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja
vya Nyerere Square.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akipata maelezo alipotembelea Banda wa Wadau wa Haki Jinai, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja vya Nyerere Square.
Bw. Laurent Burilo
akipokea Cheti cha Ushiriki wa Wizara kwenye Maonesho ya Madhimisho ya Wiki ya
Sheria kutoka kwa Kaimu Msajili wa Mahakama Mhe. Sylvester Kainda, tarehe 30 Januari, 2024 Viwanja
vya Nyerere Square.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema dunia ina imani na amani iliyoko nchini
amani ambayo inachagizwa na utawala wa sheria.
Dkt. Chana amesema hayo
alipotembelea mabanda ya maoenesho kwenye viwanja vya Nyerere Square na baadaye
kuongea na Wanahabari, tarehe 30 Januari, 2024 Jijini Dodoma.
“Dunia ina imani na Tanzania
kuhusu haki za binadamu na utawala bora ndiyo maana mkutano mkubwa wa 77 wa
haki za binadamu na watu ulifanyika Arusha mwishoni mwa mwaka 2023. Kamisheni
ya Afrika ya Haki za Binadamu hawaendi tu mahali popote, haiwezekani, bali mikutano
yao hupelekwa nchi yenye amani, isiyokuwa na vita,” amesema Dkt. Chana.
Waziri Chana aliongeza kuwa ni
kutokana na utulivu ulioko nchini, Tanzania inaandaa Mkutano mwingine mkubwa wa
Mawaziri wa Sheria wa Nchi za Jumuiya ya Madola ambao utafanyika Zanzibar
tarehe 04 – 08 Machi 2024. Mkutano ambao unategemewa kuhudhuriwa na Mawaziri wa
Sheria wasiopungua hamsini na sita.
Dkt. Chana ametumia wasaa huo
kumpongeza na kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha reforms mbalimbali kwa nia ya kuendelea kuboresha mnyororo wa
haki jinai nchini, ”Mhe. Rais ameunda Tume ya Haki Jinai ambayo imekuja na
mapendekezo mengi ambayo yameanza kutekelezwa kama tulivyoelezwa kwenye banda
la Wadau wa Haki Jinai, amekubali kufanyika kwa Kampeni ya Kitaifa ya kutoa
msaada wa Kisheria iitwayo Mama Samia Legal Aid Campaign ili wananchi wanyonge
wafikiwe kupewa elimu ya sheria na msaada wa kisheria, kutatuliwa changamoto
mbalimbali za kisheria bure, kwa kweli Mhe. Rais amedhamiria kuipeleka Tanzania
kwenye nchi ya asali na maziwa.” Alisema.
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria
yalizinduliwa rasmi tarehe 27 Januari, 2024 na Mhe. Dkt. Tulia Ackson Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yatahitimishwa Siku ya Sheria
tarehe 01 Februari, 2024 kwenye Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma ambapo
Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment