TUSHIRIKIANE KUTEKELEZA MSLAC SINGIDA: DKT. KAZUNGU
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza na Sekretarieti ya Mkoa wa Singida kufanya tathmini ya maandalizi ya MSLAC mkoani humo, 04 Januari, 2024, Singida.
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw. Stanslaus Beatus Choaji akitoa neno la
ukaribisho kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu
Kazungu ili aongee na Sekretarieti ya Mkoa, 04 Januari, 2024, Singida.
Wajumbe walioshiriki kikao cha tathmini ya maandalizi ya MSLAC mkoani Singida wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, 04 Januari, 2024, Singida.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na
William Mabusi – WKS Singida
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu ametoa wito kwa
Mkoa wa Singida kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign -
MSLAC) inayotegemewa kufanyika mkoani humo kuanzia tarehe 10 hadi 19 Januari,
2024.
Dkt.
Kazungu ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya
Mkoa wa Singida tarehe 04 Januari, 2024 kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, akiwa
ameongozana na sehemu ya Menejimenti ya Wizara. Kikao kazi hicho kililenga kufanya
tathmini ya awali ya maandalizi ya MSLAC ambayo itatekelezwa kwenye Halmashauri
zote saba mkoani humo.
“Kikubwa
ambacho Wizara inaomba kutoka kwenu ni ushirikiano mkubwa ili kufanikisha
Kampeni hii. Kote ambako tumetekeleza kampeni hii tumepata ushirikiano wa
kutosha na sasa ni zamu yenu.” Alisema na kuongeza kuwa wananchi wahamasishwe
kufika kwa wingi siku ya uzinduzi lakini pia kwenye maeneo ambayo mikutano ya
kutoa elimu na huduma ya msaada wa kisheria itakuwa inafanyika.
Akitoa
maelezo ya maandalizi yaliyofanyika kwa upande wa mkoa, Msajili Msaidizi wa
Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria mkoani humo Bi. Shukrani Mbago amesema
Halmashauri zote saba zimetaarifiwa kuhusu kufanyika kwa kampeni hiyo, Kata
zote ambazo zitapitiwa na kampeni zimeshaandaliwa, wamekaa na Watoa huduma za
kisheria, mkoa umeunda Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Kampeni. Aidha, mialiko
mbalimbali imetolewa kwa Taasisi na Wadau muhimu wanaotakiwa kushiriki Kampeni
pamoja na maandalizi ya bajeti ya kutekeleza Kampeni mkoani humo.
Akiongea
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw. Stanslaus
Beatus Choaji amesema Mkoa wake utafanya yote yanayohitajika kufanya kampeni
hiyo itekelezwe kama ilivyopangwa. Aidha, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuja na mpango huu wa
kutetea haki kwa wananchi wanyonge.
Comments
Post a Comment