TUWASHIRIKISHE WANANCHI ULINZI WA UTAJIRI ASILIA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana akizungumza na Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi
na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Utajiri na Mali Asili za nchi wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa majadiliano, Januari 18, 2024 Jijini Dar
es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na
Sheria Dr. Khatibu Kazungu akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha
Waziri wa katiba na Sheria kutoa hotuba yake, Januari 18, 2024 Jijini Dar es
Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na Lusajo Mwakabuku -
WKS Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amewataka Viongozi wa umma wenye jukumu la
kusimamia Utajiri Asili na Mali Asilia za nchi kuwashirikisha wananchi katika
kulinda rasilimali hizo ili kuhakikisha zinalinufaisha taifa na wananchi kwa
ujumla wake.
Dkt. Chana amesema hayo Januari
18, 2024 jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa majadiliano
uliowakutanisha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Wadau mbalimbali wa Sekta
ya Utajiri na Mali Asili za nchi kwa lengo la kuwajengea uelewa wa kusimamia na
kufanya uangalizi wa utajiri asili na mali asilia za nchi.
Aidha, Waziri Dkt. Chana amesema
mafunzo hayo yatasaidia kuongeza maarifa ya kuwawezesha watumishi hao kusimamia
vyema rasilimali za nchi ili kuvutia uwekezaji utakaoleta manufaa kwa taifa na
wananchi ambapo pia amewataka watumishi hao kuja na mikakati na kuishauri
Serikali kuhusu utajiri asili na mali asilia za nchi.
"Dhamira hii inaenda
sambamba na matakwa ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambayo inasisitiza
kusimamia uwekezaji wa sheria za kulinda rasilimali za taifa na kuboresha sera
na sheria zinazohusu ulinzi, uendelezaji, uwekezaji katika rasilimali za taifa
hususan kusimamia utekelezaji wa sheria za kuwezesha majadiliano kwenye
mikataba ya uwekezaji katika utajiri asili na mali asilia za nchi." Alisema
Waziri Dkt. Pindi Chana
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri na Mali Asilia za Nchi Kamishna wa Polisi
Neema Mwanga amebainisha kuwa ipo haja ya kuweka misingi imara ya kisheria na
usimamizi wa rasilimali asilia ambazo zitasaidia kuvutia wawekezaji.
"Sheria hizi zinatutaka
tusiingie mikataba isipokuwa tu pale ambapo tunahakikisha wananchi watafaidika,
kuna njia nyingi ambazo wananchi wanaweza kunufaika na rasilimali hizi, wengine
kwa kupata ajira na wengine watafaidika kwa kuingia mikataba midogo midogo kama
vile usambazaji wa vyakula katika miradi inayoendeshwa"
Comments
Post a Comment