WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bi. Fatuma Ramadhan Mganga akihutubia wakati alipofungua Mafunzo ya Siku moja ya namna ya kutekeleza MSLAC mkoani humo, 09/01/2024.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Msaada wa Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Bi.
Ester Msambazi akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa MSLAC, tarehe 09/01/2024,
Singida.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Siku moja ya namna ya kutekeleza MSLAC wakimsikiliza Mgeni Rasmi, tarehe 09/01/2024, Singida.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida Bi. Fatuma Ramadhan Mganga kwenye picha ya pamoja na
baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Siku moja ya namna ya kutekeleza MSLAC,
tarehe 09/01/2024, Singida.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na William Mabusi –
WKS Singida
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Singida Bi. Fatuma Ramadhan Mganga ametoa wito kwa Wataalam watakaoshiriki
Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ijulikanayo kama Mama Samia Legal Aid
Campaign mkoani humo wanaitekeleza kwa kutoa maamuzi na ushauri sahihi kwa wananchi
watakao wahudumia ili kuwawezesha kupata haki zao.
Bi. Fatuma ametoa wito huo
wakati akifungua Mafunzo ya Siku moja ya namna ya kutekeleza MSLAC mkoani humo
yaliyowashirikisha watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo Wanasheria, Maafisa
ardhi, Maafisa maendeleo ya jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri
zote saba za mkoa wa Singida na Taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, tarehe 09
Januari, 2024 ofisi za Mkuu wa Mkoa.
“Mnaenda kutoa elimu na
kutatua changamoto za wananchi zinazohusu masuala ya sheria, wasikilizeni kwa
makini, wachukulieni kama wateja, wajengeeni imani na kuwapa muda wakujieleza
ili wafunguke kueleza changamoto zao, ni kwa kuwaelewa ndiko kutakakowasaidia
kutoa maamuzi sahihi.”
Akibainisha upekee wa Kampeni
hiyo Bi. Fatuma amesema “Kampeni hii ni ya kipekee sana kwani inaenda kumpa
haki baba ambaye kwa muda mrefu amenyang’anywa haki yake na familia yake kuishi
kwa mateso, inaenda kumpa haki mama ambaye kwa muda mrefu alikosa haki yake ya
mirathi.” Huku akikumbusha pia watoto wasiachwe kusikilizwa kwani yamkini
kampeni ikabaini watoto ambao wamekuwa wakinyimwa haki ya shule, kuishi katika
ukatili ama kubakwa.
Aidha, ameomba ushiriki wa
kutosha kwa Vyombo vya Habari ili kufikisha ujumbe kwenye maeneo ambayo
hayatafikiwa na Kampeni, kupitia Vyombo vya Habari Wananchi katika maeneo hayo
wataweza kufikisha malalamiko yao kwa njia ya simu au kupitia njia nyingine
rasmi na malalamiko hayo yakafanyiwa kazi.
Awali akitoa maelezo kuhusu
utekelezaji wa MSLAC, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Msaada wa Kisheria na
Msajili wa Watoa huduma za msaada wa kisheria, Bi. Ester Msambazi amesema
Singida ni mkoa wa Sita tangu kuanza kutekelezwa kwa kampeni hiyo na lengo la
kutekeleza MSLAC ni pamoja na kuziba ombwe lililopo la wananchi kutotambua sheria
na wapi waende wanapokuwa na changamoto za kisheria.
Utekelezaji wa kampeni hiyo
unaohusisha kutoa elimu ya masuala ya sheria, msaada wa kisheria na kutoa
huduma za msaada wa kisheria kwa Wananchi wote na hasa wasio na uwezo wa kumudu
gharama za Mawakili utazinduliwa Rasmi mkoani humo tarehe 10 Januari, 2024 na
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, na itatekelezwa kwa
siku kumi.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria
ya Mama Samia ilizinduliwa Rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 27 April 2023 na hadi sasa imeshatekelezwa katika mikoa mitano ambayo ni
Dodoma, Manyara, Shinyanga Ruvuma na Simiyu na huu unakuwa ni mkoa wa Sita.
Comments
Post a Comment