WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO CHA KIMKAKATI NA MENEJIMENTI YA WIZARA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara kilichofanyika Mtumba leo tarehe 24 Januari, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Pindi Chana akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Wizara kilichofanyika
Mtumba leo tarehe 24 Januari 2024 jijini Dodoma.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na, George Mwakyembe – WKS Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya
kikao na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na kupokea taarifa
mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Kikao hicho kimefanyika leo
tarehe 24 Januari, 2024 katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma
kikiwa na malengo ya kutathmini kwa kina utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa
nusu muhura wa bajeti ya mwaka 2023/ 2024.
Mhe. Waziri Chana ameiopongeza
Menejimenti na watumishi wote kwa ujumla kwa kazi kubwa wanayofanya katika
kuhakikisha kazi za kuwahudumia wanachi zinakwenda vizuri na kwa wakati.
Akiongea kwenye kikao hicho
Waziri Chana amesema “natambua jukumu la kutekeleza majukumu haya ni kubwa
lakini lazima tuongeze kasi ya kujituma zaidi kuhakisha tunatimiza adhima ya
Mhe Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya
kuwahudumia watanzania ikiwemo kutatua kero mbalimbali”.
Comments
Post a Comment