WAZIRI CHANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA UNICEF TANZANIA


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akifafanua jambo wakati wa kikao na Mwakilishi Mkuu wa UNICEF nchini Bi, Elke Wisch kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 jijini Dodoma. 

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akipeana mikono na mwakilisha mkuu wa shirika la UNICEF nchini Bi, Elke Wisch baada ya kikao kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma.

 


   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Pindi Chana akiwa kwenye picha ya  pamoja na Mwakilishi Mkuu wa UNICEF nchini Bi, Elke Wisch baada ya kikao kilichofanyika leo tarehe 30 Januari 2024 Jijini Dodoma.

 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na, George Mwakyembe -  WKS Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la kuhudumia watoto nchini (UNICEF) Bi, Elke Wisch na kujadili masuala mbalimbali kuhusu haki za watoto.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika leo tarehe 30 Januari 2024 jijini Dodoma, Mhe Chana ameishukuru Unicef kwa kazi kubwa wanayofanya hapa nchini pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na UNICEF.

Aidha, Mhe Chana amefafanua kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulinda haki za watoto   ikiwemo kupinga sheria ya mtoto ya kuruhusu kuolewa ifikapo umri wa miaka 18 (The marriage Act, 1971). Mhe Chana ameongeza kuwa tayari Serikali imepeleka mswada bungeni ili kuongeza umri wa kuoa na kuolewa na kuondoa tatizo la ndoa za utotoni.

Vilevile Mhe. Chana amelezea kuwa kupitia kampeni ya Mama Samia msaada wa Kisheria ambayo imekuwa ikitoa elimu dhidi ya ukatili wa watoto imekuwa msaada mkubwa sana kwa watanzania kwani asilimia kubwa sasa wamejua haki za watoto na wanazitekeleza.

“Mama Samia Legal Aid Campaign imekuwa imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuelimisha wananchi haki za watoto, lakini pia kunga ukatili dhidi ya watoto lakini pia hata wakina mama, na watanzania wamekuwa wanatuelewa na kuishukuru Serikali kwa kampeni hii,” Alisema Waziri Chana. 

Naye Mwakilishi Mkuu wa shirika la watoto hapa nchini (UNICEF) Bi, Elke Wisch ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano mzuri wanaowapa, lakini pia kwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda haki za watoto na kupinga ukatili wa watoto.

Bi Elke amesema “Kitendo cha Serikali kuruhusu watoto wakike waliopata mimba kurudi shule ni ishara tosha ya kuwa Serikali inasimamia haki za watoto” Bi Elke pia mefafanua kuwa, kwa sasa serikali iangalie zaidi kwenye usafirishaji haramu wa watoto ambao umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

UNICE ni Shirika linalohudumia watoto na wanawake duniani ambalo limeanzishwa mwaka 1946 makao makuu yake yakiwa New York nchini Marekani, kazi kubwa ya shirikia hili ni kutoa huduma za Maendeleo  kwa watoto na wanawake  duniani.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA