WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA TAASISI YA USULUHISHI TANZANIA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya usuruhishi nchi(Tanzania Institute of Arbitrators ) pamoja na Watumishi wa Wizara  kwenye kikao kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma.



Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akitoa ufafanuzi kwenye  kikiao na viongozi wa Taasisi ya usuruhishi (Tanzania Institute of   Arbitrators) kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana akipokea vitabu kutoka kwa Makamu wa Rais wa Taasisi  ya Usuruhishi Ndg, Anderickson Njunwa kwenye kikiao kilichofanyika leo tarehe 29 Janauri 2024 jijini Dodoma.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na, George Mwakyembe - WKS Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya kikao na viongozi kutoka Taasisi ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara kwa Njia Mbadala - TIARB (Tanzania Insitute of Arbitrators) na kujadili masuala mbalimbali ya namna ya kutatua migogoro kwa njia ya mapatano badala ya kwenda mahakamani.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 29 Januari 2024 jijini Dodoma, Mhe Balozi Chana amesema ni vyema taasisi hiyo ikaweka nguvu kubwa  katika kujitangaza (Branding) ili wananchi waweze kujua na kutambua umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia ya amani. 

“Kutatua migogoro nje ya Mahakama kunajenga ushirikiano kwenye jamii zetu lakini pia kunaondoa chuki baina ya wagombanao, ni gharama nafuu pamoja na inachukua muda mfupi. Hivyo ni lazima kuwaeleza na kuwaeleimisha watanzania kutumia njia hizi za utatuzi wa migogoro badala ya kukimbilia mahakamani” Alisema Waziri Chana.

Naye, Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo Ndg, Anderickson Njunwa alieleza kuwa wao kama taasisi wamejipanga kuhakikisha watoa elimu kwa watanzania pamoja na semina mbalimbali za namna ya kutatua migogoro kwa njia ya upatanishi na mashauriano  ili kupunguza kesi mahakamani lakini pia kujenga upendo na  ushirikiano  katika jamii zetu.

Akiongelea mikakati mbalimbali ambayo taasisi hiyo inaendelea kuitekeleza, Bwana Njunwa alisema kwa mwaka huu tayari wameweka mkakati wa kuendesha semina na mikutano mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo wasuruhishi pamoja na watatuzi wa mogogoro.

Taasisi ya Usuluhishi Tanzania (TIArb) ilisajiliwa Desemba 1999 na Msajili wa Vyama kwa Cheti cha Usajili Namba 8833. Kazi kubwa ya TIArb ni kukuza na kuwezesha utatuzi wa migogoro ya kibiashara nchini Tanzania. Kabla ya kuanzishwa kwake, Baraza la Kitaifa la Ujenzi (NCC) lilikuwa likichukua jukumu kama hilo kwa migogoro inayohusiana na ujenzi pekee. 



 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA