BAJETI ZIZINGATIE UTEKELEZAJI WA 4R ZA MHE. RAIS – DKT. CHANA

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea alipokutana na Wakuu na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma.


Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Bw. George Mandepo akitoa wasilisho fupi la maoteo ya bajeti ya Taasisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma.


Kabidhi Wasii Mkuu ofisi ya RITA Bw. Frank Kanyusi akitoa wasilisho fupi la maoteo ya bajeti ya Taasisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25, tarehe 06 Februari, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameziagiza Taasisi za Wizara hiyo kuhakikisha zinazingatia pamoja na mambo mengine ya maendeleo lakini pia utekelezaji wa R4 za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Chana ametoa agizo hilo wakati alipokutana na Wakuu wa Taasisi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara, Wakurugenzi kutoka Wizarani na kupitishwa kwenye maoteo ya Bajeti ya mwaka fedha 2024/25 kwa Taasisi hizo tarehe 06 Februari, 2024 kwenye ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

”Katika kipindi hiki cha kukamilisha maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 kila Taasisi na Mkuu wa Taasisi atwambie namna ambavyo amejipanga kuzitekeleza zile R4 za Mhe. Rais. Pangeni kufanya mageuzi na maboresho makubwa kwenye matumizi ya TEHAMA, Kufanya tathmini na mapitio ya sheria mbalimbali, Kuongeza visibility kwa maana ya kutangaza Taasisi zenu na Kuendelea kutoa elimu kwa umma, Kuwajengea uwezo watumishi.” Alisema Dkt. Chana huku akihimiza pia Taasisi hizo kuongeza mashirikiano na Wadau wa Maendeleo kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA