TUNAANDAA MKUTANO WA VIWANGO VYA JUU – DKT. CHANA

 


Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amepitishwa kwenye taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sheria kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, tarehe 05 Februari, 2024 Dodoma na kuahidi “Tutafanya Maandalizi mazuri na kwa Viwango vya Kimataifa kwa heshima ya Nchi yetu.”

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amepitishwa kwenye taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sheria kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, tarehe 05 Februari, 2024 Dodoma na kuahidi kuandaa mkutano utakaokuwa wa viwango vya juu kwani tayari uwezo wa kuandaa mikutano ya kimataifa Wizara unao ambapo mwishoni mwa mwaka 2023 Wizara iliratibu kikao cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binafamu kilichofanyika mkoani Arusha kwa siku 21.

“Tutafanya Maandalizi mazuri na kwa Viwango vya Kimataifa kwa heshima ya Nchi yetu.” Alisema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Katiba na Sheria akilezea mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 04 – 08 Machi, 2024 Zanzibar.



Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA