DKT. CHANA ASISITIZA UADILIFU
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Mbuki Feleshi akihutubia kabla ya kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria kufunga Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, tarehe 22 Machi, 2024 Jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria waliokuwa wanashiriki Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, baada ya kupiga kura ya kuwachagua viongozi mbalimbali wa Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 22 Machi, 2024 Jijini Dodoma.
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewaagiza Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria
kuzingatia utawala wa sheria na kuendelea kuwa waadilifu katika utekelezaji wa
majukumu yao ili kuwajenga imani wananchi wanowatumikia.
Dkt. Pindi ameyasema hayo
alipokuwa anafunga Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliokuwa unafanyika
kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 22 Machi, 2024.
“Endeleeni kuwa waadilifu na
kuwajengea imani wananchi ya kuwaamini watumishi wa umma, nendeni na wazo moja
tu la kuwatumikia wananchi kwa weledi, katoeni ushauri wenye tija kisheria
kwenye maeneo yenu ya kazi, lazima uwepo wa Wakili au Mwanasheria mahali fulani
utambulike.” Alisema.
Aidha, Dkt. Pindi amewashauri
Mawakili hao wa Serikali kujiendeleza ili kuongeza maarifa akiyataja maeneo ya
kipaumbele kuwa ni pamoja na elimu ya Uandaaji
wa mikataba ya kimataifa, Usuluhishi wa mgogoro kwa njia mbadala (Alternative
Dispute Resolution - ADR) na Matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligent).
Kuhusu utekelezaji wa Kampeni
ya Kitaifa ya utoaji wa msaada wa kisheria ya Mama Samia inayoendelea
kutekelezwa kote nchini kwa miaka mitatu tangu ilipozinduliwa Aprili, 2023, amesema
Wizara yake inakwenda kuanzisha directory ya Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria
ili wajuane na kutambuana katika maeneo yao akiwataka wawe tayari kupokea na
kukabiliana na changamoto za wananchi huko walipo, kwani watanzania zaidi ya
milioni 61 wanahitaji huduma yao.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Mbuki Feleshi amesema faraja yake
ni ustawi wa Mawakili wa Serikali na kuwa yeye ni muumini wa ubora na weledi hivyo
ofisi yake itafanya kadri itakavyoweza kuona Mawakili wa Serikali wanakuwa wa
viwango vya juu, huku akiwataka kujifunza mambo mengine kutoka kwa wazee
akimaanisha yeye mwenyewe na viongozi wengine wa ngazi za juu katika sekta ya
sheria.
Mkutano huo Mkuu wa Mawakili
wa Serikali ulikuwa wa siku tatu, ulianza tarehe 21 Machi, 2024 ambapo
ulifunguliwa rasmi tarehe 22 Machi, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Comments
Post a Comment