JUKUMU LA WANANCHI KUPATA HAKI NI LENU – WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, 21
Machi, 2024 Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akipokea Miongozo mbalimbali ikiwemo ya Uandishi wa Sheria na Utoaji wa Huduma ya Msaada wa Kisheria iliyozinduliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali, 21 Machi, 2024 Dodoma.
Wakurugenzi wa Wizara ya
Katiba na Sheria ambao pia ni Mawakili wa Serikali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu
wa Mawakili wa Serikali, tarehe 21 Machi, 2024 Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS
Dodoma
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb)
amesema Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria nchini ni jukumu lao kutoa haki
kwa wananchi katika kuimarisha misingi ya haki na utawala bora.
Mhe.
Majaliwa ametoa kauli hiyo alipokuwa anafungua Mkutano Mkuu wa siku tatu wa
Mawakili wa Serikali tarehe 21 Machi, 2024 Jijini Dodoma.
”Serikali
inaendela kuchukua hatua za maksudi na madhubuti kuboresha mfumo wa haki jinai,
kujenga mazingira wezeshi kwa Mawakili wa Serikali na Maafisa wa Sheria ya
kutoa huduma za kisheria kwa wananchi kote nchini, hivyo ni jukumu lenu kutoa
haki kwa wananchi kwa wakati na pasipo kujali dini yake, rangi yake au itikadi
ya siasa kwani kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watu
wote ni sawa mbele ya sheria na wote wanapashwa kulindwa na kupata haki sawa,”
amesema Mhe. Waziri Mkuu.
Akiongelea
uhitaji wa huduma ya sheria amesema ”katika miaka ya hivi karibuni jamii
imepitia mabadiliko na maendeleo mbalimbali katika maeneo ya kiuchumi,
kiteknolojia, kiasiasa na kiutamaduni. Maendeleo hayo yameongeza uhitaji wa
upatinakaji wa huduma za kisheria.”
Akihitimisha
hotuba yake Mhe. Majaliwa amewaagiza Mawakili wa Serikali na Maafisa Sheria
kutekeleze majukumu yao ya kisheria kwa uadilifu, weledi, uwajibikaji,
uaminifu, usiri, umakini na kwa kujituma huku akiwata kushirikiana na Wizara ya
Katiba na Sheria katika kutekeleza kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia
Lega Aid Campaign kwa kuipa uzito kama majukumu yao mengine ya kila siku.
Aidha,
ameziagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Taasisi zingine za utoaji haki kufungua na
kuimarisha ofisi katika ngazi za chini ili kuhakikisha huduma za kisheria
zinawafikia wananchi wengi.
Awali
akihutubia kwenye mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameyataja matunda ya kazi
wanazofanya Mawakili wa Serikali akisema “katika miaka miwili ya kuwepo kwa
Chama cha Mawakili tunashuhudia mchango mkubwa wa Mawakili wa Serikali katika
sekta ya sheria ambao umewezesha ustawi wa masuala ya kiuchumi, kijamii, kisiasa,
uwekezaji, utalii, uhusiano wa kimataifa, utoaji haki, utawala wa sheria, umoja
wa kitaifa, na msaada wa kisheria, yote ni matunda ya uwepo wa Mawakili wa
Serikali wenye ueledi na ufanisi katika kuchapa kazi.”
Akitaja
mafanikio ya miaka mitatu ya Mhe. Rais hususan kwenye sekta ya sheria amesema
”miaka mitatu ya Dkt. Samia tumeona kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai ambayo baada
ya kazi yake imetoa mapendekezo ya namna ya kuboresha mfumo wa utoaji haki na sasa
mapendekezo hayo yameanza kutekelezwa na ofisi nyingi za Serikali,” ameyataja
mafanikio mengine kuwa ni kuendelea kutolewa kwa msaada wa kisheria kwa
wananchi hasa wanyonge kupitia Kampeni ya Kitaifa ya Mama Samia Legal Aid
Campaign, hivyo akatoa rai kwa wanasheria kutimiza wajibu wao wa kuwasikiliza
watanzania, kwaelekeza na kuwasidia kupata huduma ya sheria na hapo watakuwa
wameitendea haki Kauli mbiu ya mkutano huo inayosema “Upatikanaji wa huduma za kisheria kwa
Wananchi ni nguzo kwa ustawi wa jamii.”
Comments
Post a Comment