KAMATI YAIPONGEZA SERIKALI UJENZI WA JENGO LA WAKILI MKUU WA SERIKALI
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Mark Mulwambo akitoa maelezo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 27 Machi, 2024 Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Mkandarasi wa mradi Eng. Baraka Mosha akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Wakili Mkuu wa Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 27 Machi, 2024 Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo, viongozi kutoka Wizarani na
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mbele ya jengo la Wakili Mkuu wa Serikali linalojengwa
Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, tarehe 27
Machi, 2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS
Dodoma
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe.
Florent Kyombo ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya za kuendelea
kukamilisha majengo ya kudumu ya Wizara na Taasisi za Serikali kwenye eneo la
Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma.
Mhe.
Kyombo amesema hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa Jengo la kudumu
la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 49,
tarehe 27 Machi, 2024 eneo la Mtumba kunakojengwa Mji wa Serikali.
“Tunaipongeza
Serikali kwa kuendelea kutenga bajeti ya kujenga majengo makubwa kama hili la
Wakili Mkuu wa Serikali, kiu yetu ni kuona jengo hili linakamilika na kuanza
kutumika kama ilivyokusudiwa. Hivyo tuiombe Serikali kuongeza kasi ya malipo kwa
Mkandarasi na Msimamizi wa mradi kuwawezesha kufanya kazi ili mradi huu
ikamilike kwa muda uliopangwa.” Alisema.
Katika
ukaguzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo
aliyemwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana,
amesema Wizara itaendelea kufanya kazi kwa kusaidiana na kumshauri Mshitili
ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali katika kukabiliana na changamoto zozote kwenye
ujenzi huo.
Awali
akitoa taarifa ya ujenzi, Mkandarasi wa mradi huo Eng. Baraka Mosha amesema ujenzi
unaendelea vizuri pamoja na kuwepo changamoto kadhaa ikiwemo kuchelewa kwa
malipo.
Akijibu
baadhi ya hoja, Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Mark Mulwambo
amesema ofisi yake imeingia makubaliano na Mkandarasi kutumia mpango wa
Manunuzi wa Milestone, mpango ambao utawezesha upatikanaji wa pesa kabla ya
kazi kufanyika, badala ya mpango wa Mkandarasi kulipwa kwa Certificate baada ya
kufanya kazi.
Comments
Post a Comment