RAIS MWINYI AFUNGA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI ZA MADOLA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati anafunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola MH. Patricia Scotland KC, 08 Machi, 2024 Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kabla ya kufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu (kulia) miongoni mwa Viongozi waliohudhuria hafla ya kufunga Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, 08 Machi, 2024 Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola MH. Patricia Scotland KC, kulia kwake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo baada ya kuongea na Wanahabari, 08 Machi, 2024 Zanzibar.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi WKS – Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefunga Mkutano wa
Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na kuzitaka nchi
wanachama kutumia teknolojia na kuhakikisha haki inawafikia wote bila kuyasahau
makundi maalum.
Mkutano huo wa Siku tano
uliokuwa unafanyika Visiwani Zanzibar ukiongozwa na Mwenyekiti Waziri wa Katiba
na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, umefungwa
rasmi leo tarehe 08 Machi, 2024.
“Nchi wanachama tujitahidi
kuhakikisha haki inaendelea kutolewa kwa wote na sasa kwa kuwa nchi wanachama
umeazimia kujikita katika kutumia teknolojia haki iwafikie makundi maalum
wakiwemo walemavu. Amesema Dkt. Mwinyi huku akisisitiza umuhimu wa matumizi ya
namna nyingine ya mawasiliano yakiwemo matumizi ya alama kwa watu wenye
changamoto ya usikivu.
Akisoma taarifa ya mkutano huo
kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa
Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda Mhe. Dkt. Emmanuel Ugirashebuta
amesema “Mawaziri wa Sheria wamepokea na kujadili maudhui yanayohusiana na
teknolojia na uvumbuzi ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama za kuendesha
mashtaka na kurahisisha mchakato wa kisheria katika upatikanaji wa haki. Umoja
ni nguvu, tutaendelea kushirikiana katika maeneo yote tuliyokubaliana katika
majadiliano wakati wa mkutano.”
Akiongea kwenye mkutano ulioandaliwa
wa Wanahabari Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola MH. Patricia Scotland KC ametoa
shukrani zake za dhati kwa nchi ya Tanzania na Zanzibar kwa kuuratibu vyema
mkutano huo ambao lengo lake ni kudumisha umoja miongoni mwa nchi wanachana.
“Mkutano huu umekuwa ni wenye mafanikio makubwa, tunaelewa miongoni mwa nchi wanachama zimo nchi ambazo zimepiga hatua kimaendeleo, zipo ambazo zinaendelea, kuna nchi kubwa na ndogo hivyo tutumie kile tulichonacho kuwanufaisha wanachama wengine” alisema na kuagiza uzingatiaji wa utoaji wa haki kwa kuyafikia maeneo ya pembezoni akiitaja kampeni ya Mama Samia ambayo sasa imeshika kasi kote Tanzania Bara na Zanzibar kama mfano.
Comments
Post a Comment