DKT. CHANA AMPOKEA JUMANNE SAGINI

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi ua la ukaribisho Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini alipowasili Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya hafla ya uapisho iliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024. Anayeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Mary Makondo.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na viongozi wa Wizara na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo mara baada ya kumkaribisha na kumpokea Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Jumanne Sagini katika mapokezi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa Ikulu, tarehe 04 Aprili, 2024.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza na Viongozi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo mara baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. 04 Aprili, 2024.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo akizungumza na Viongozi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakati akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amkaribishe Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Jumanne Sagini ili azungumze na viongozi hao. 04 Aprili, 2024.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo. 04 Aprili, 2024.

Viongozi wa Wizara na Taasisi za Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Balozi Pindi Chana (hayupo pichani) baada ya hafla ya kuapishwa Ikulu kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Jumanne Sagini Jijini Dar es Salaam. 04 Aprili, 2024.


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini akisalimiana na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali alipowasili Ofisini hapo mara baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam. 04 Aprili, 2024.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA