SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MAJENGO YA MAHAKAMA
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akijibu maswali Bungeni tarehe 02
Aprili, 2024 Jijini Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na
William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaendelea
kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kujenga majengo mapya na kukarabati majengo chakavu.
Dkt.
Chana amesema hayo wakati akijibu maswali Bungeni leo tarehe 02 Aprili, 2024
Jijini Dodoma.
”Serikali
kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imeendelea kuimarisha majengo ya
Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na
kukarabati majengo chakavu kwa awamu kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti.” Amesema
Dkt. Chana akijibu swali la Mhe. Francis
Isack Mtinga Mbunge wa Wilaya ya Mkalama aliyetaka kujua ujenzi wa Mahakama kwenye
Wilaya hiyo utaanza lini.
Mhe.
Waziri amesema Wilaya ya Mkalama ambayo ni moja ya Wilaya nne ambazo bado
huduma za Mahakama zinapatikana kupitia Wilaya za jirani imo kwenye mpango wa
Mahakama zitakazojengwa katika Bajeti ya Mwaka 2023/24 ambapo maandalizi ya
michoro ya Mahakama hiyo yamekamilika na zabuni imetangazwa ili kupata Mkandarasi
wa ujenzi.
Amezitaja
Mahakama zingine ambazo zimo kwenye mpango wa bajeti ya mwaka 2023/24 kuwa ni
pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Kishapu na Tarime.
Akijibu
swali la nyongeza kutoka kwa Mhe. Asha Abdallah Juma aliyeteka kujua mpango wa
Serikali wa kuwa na kitengo ama hotline kushughulikia malalamiko ya Wananchi
wanaopata shida na usumbufu kufuatilia kesi zao
Dkt. Chana amesema tayari Mahakama ina namba maalum 0752 500 400 ambayo
mwananchi anaweza kupiga kupata taarifa za kesi yake pamoja na malalamiko
mengine.
Comments
Post a Comment