UKATILI WOWOTE WANAOFANYIWA WATOTO UTOLEWE TAARIFA – DKT. CHANA

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, 05 Aprili, 2024 Jijini Arusha.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akitoa salaam na kumkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kuhutubia Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, 05 Aprili, 2024 Jijini Arusha.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Ester Msambazi akitoa wasilisho kwenye Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, 05 Aprili, 2024 Jijini Arusha.

Sehemu ya Washiriki kwenye Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. 05 Aprili, 2024 Jijini Arusha.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja na washirki wa Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto, kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu. 05 Aprili, 2024 Jijini Arusha.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lusajo Mwakabuku – WKS Arusha

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka watanzania hususan Vyombo vya Habari kuongeza juhudi katika kuwalinda Watoto kwa kutoa taarifa za ukatili unaofanyika dhidi yao  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Mhe. Chana ameyasema hayo leo tarehe 05 Aprili, 2024 wakati akihutubia Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Four Points Jijini Arusha huku akiwataka washiriki kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika kuhakikisha haki kwa watoto inapatikana.



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA