WAZIRI PINDI AKUTANA NA BALOZI WA SINGAPORE
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana wakati anaongea na Balozi wa
Singapore nchini Mhe. Douglas Foo,
Aprili 22, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa na Mgeni wake Balozi wa Singapore nchini Mhe. Douglas Foo baada ya kufanya mazungumzo, Aprili 22, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi zawadi Mgeni wake Balozi
wa Singapore nchini Mhe. Douglas
Foo baada ya kufanya mazungumzo, Aprili 22, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni wake Balozi wa Singapore nchini Mhe. Douglas Foo baada ya kufanya mazungumzo, Aprili 22, 2024 Bungeni Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Balozi wa Singapore nchini Mhe.
Douglas Foo, kwenye picha
ya pamoja na watumishi wengine walioshiriki kikao hicho Aprili 22, 2024 Bungeni
Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Singapore nchini Mhe. Balozi Douglas Foo ambapo wameongelea na kukubaliana
maeneo mbalimbali ya kufanya mafunzo na kubadilishana uzoefu.
Mazungumzo hayo yamefanyika Aprili 22,
2024 Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maazimio ya
Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika
mwezi Machi 2024 Zanzibar. Katika mkutano huo moja ya maazimio yaliyopitishwa
ni nchi wanachama kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali ikiwemo sheria, teknolojia
na matumizi ya akili bandia.
Katika mazungumzo ya leo Mhe. Foo amesema
Singapore iko tayari kutoa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala,
suala ambalo limepokelewa kwa mikono miwili na Dkt. Chana. “Kama Wizara tunaona umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa
njia mbadala na tunaendelea kufungua Vituo vya Utatuzi wa Migogoro kwa mjia
Mbadala nchini. Nimependezwa na ajenda hii muhimu ya mafunzo na imekuja kwa muda
muafaka.”
Maeneno
mengine ya kujifunza na kubadilishana uzoefu waliyokubaliana ni usalama wa taarifa
za mtandaoni na mifumo ya TEHAMA, ushirikiano kwenye Taasisi za sheria kama Chama
cha Wanasheria Tanganyika na Taasisi za Mafunzo ya Sheria.
Comments
Post a Comment