BUNGE LAIDHINISHA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya
pamoja na watumishi wa Wizara na Taasisi zake waliohudhuria kikao cha Bunge, Aprili
29, baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2024/25.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Yasinta Kissima na William Mabusi – WKS Dodoma
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kuidhinisha Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Akiwasilisha
Bajeti hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Bungeni
Jijini Dodoma Aprili 29, 2024 amesema kuwa, katika mwaka wa fedha 2024/25 Wizara inataraji kutumia jumla ya Shilingi Bilioni 441.26.
Akiwasilisha
makadirio ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha
2024/2025 Mhe. Balozi Pindi Chana amesema kuwa kati ya fedha hizo
Shilingi Bilioni 112.4 ni kwa ajili ya
mishahara ya Watumishi, Shilingi Bilioni 223.16 ni kwa ajili ya matumizi
mengineyo na Shilingi Bilioni 105.67 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya
maendeleo.
Katika
hotuba yake Dkt. Pindi Chana amesema kuwa kwa
mwaka wa fedha 2024/25 Wizara na Taasisi zake zitaendelea kuboresha
utoaji wa huduma za Sheria na utoaji wa haki kwa umma ili kuendana na Mipango
ya Sekta ya Sheria nchini na Mipango ya Kikanda na Kimataifa ili kufikia
malengo yanayotarajiwa.
Comments
Post a Comment