Posts

Showing posts from May, 2024

WANANCHI LUPILA WAITWISHA MSLAC KERO YA WANYAMA WAHARIBIFU

Image
  Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Zakaria Mzese akitoa elimu ya Sheria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila Mei 30, 2024 Makete. Afisa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Bw. Francis Malembo akitoa mada ya wanyamapori na makatazo kwenye Hifadhi za Taifa na Mapori Tengefu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila Mei 30, 2024 Makete. Mwanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fredrick Makamba akitoa mada ya ndoa na talaka kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila Mei 30, 2024 Makete. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WKS Makete Wananchi wa Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila Wilayani Makete wameitwisha Timu inayotekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Wilayani humo kero ya wanyama nyani na ngedere ambao wamekuwa tishio kwa kuharibu mazao na kutishia amani. Malalamiko hayo yametolew...

MSLAC KUTOA ELIMU MKESHA WA MWENGE – DC MAKETE

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Makete Bw. Juma Sweda akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Mei 29, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa MSLAC. Mkuu wa Wilaya ya Makete Bw. Juma Sweda (wa pili kushoto) akisikiliza uwasilishwaji wa mada kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Mei 29, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa MSLAC. Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete Bw. William Makufwe akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Mei 29, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa MSLAC. Mwanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fredrick Makamba akitoa mada ya sheria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Mei 29, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa MSLAC. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Makete Mkuu wa Wilaya ya Makete Bw. Juma Sweda amefurahishwa na utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayoendelea kutek...

"MSLAC ITUSAIDIE. KUNA MIGOGORO IMETUSHINDA" – DC KISSA

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima – WKS Njombe Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Kasongwa amesema kuwa kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika Wilaya ya Njombe ipo migogoro ya muda  mrefu ambayo imekuwa ikijadiliwa na kuhamishiwa kwa Viongozi mbalimbali lakini ufumbuzi wa migogoro hiyo umekuwa haupatikani. Mhe. Kissa aliyasema hayo Mei 29, 2024 wakati akiwasilisha salamu za Serikali katika Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe uliofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Halmashauri yaliyopo Kijiji cha Kidegembye  Kata ya Lupembe Wilayani Njombe. "Tunaupongeza uongozi wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye chini ya uratibu wa Wizara ya Katiba na Sheria waliamu kuja na ubunifu wa kuleta huduma za Kisheria za bure Mama Samia Legal Aid Campaign. Kuna mifupa huko imetushinda Waheshimiwa Madiwani. Zipo kesi za miaka mingi sana Wananchi wanahamisha malalamiko kwa Viongozi mbalimbali kila anap...

MSLAC IMESAIDIA KUSUKUMA MASHAURI MENGI YA JINAI – DPP MWAKITALU

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima-WKS Njombe Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Sylvester Mwakitalu, amesema kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imesaidia kusukuma mashauri mengi ya jinai kutokana na malalamiko na mapendekezo ambayo wamekuwa wakiyapokea kutoka kwa wadau wao. Mwakitalu aliyasema hayo mjini Njombe mara baada ya kutembelea katika Gereza la Njombe na kuzungumza na mahabusu na wafungwa waliopo katika Gereza hilo. "Katika mikoa ambayo kampeni hii imeshafanyika na sasa katika mkoa wa Njombe, tumekwenda kwenye Magereza, tumekwenda kwenye mahabusu za watoto kuna mambo mengi yameibuka na mengi tumeyafanyia kazi. Zipo baadhi ya kesi zimesimama haziendelei, kutokana na sababu mbalimbali lakini baada ya kusikia na kupokea malalamiko na maelekezo kutoka kwa wadau mengi tumeyapatia ufumbuzi."Alisema Mwakitalu DPP Mwakitalu amesema kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria imesaidia sana kusukuma mashauri mengi ya Jinai kwa wateja wanaowahudumia ikiwa ni p...

MSLAC YAWAFUTA MACHOZI WALIOSHINDWA KUMUDU GHARAMA ZA MAWAKILI

Image
  Wananchi wa Kijiji cha Nundu Kata ya Yakobi Halmashauri ya Mji Njombe wakipatiwa huduma ya msaada wa kisheria. Mei 28, 2024 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima – WKS Njombe Wananchi wa Kijiji cha Nundu Kata ya Yakobi Halmashauri ya Mji Njombe wamepongeza ujio wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutokana na huduma hiyo kutolewa bila malipo, ambapo awali Wananchi walidhulumiwa haki zao kutokana na wengi kushindwa kumudu gharama za Mawakili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti mara baada ya timu ya wataalam wa msaada wa kisheria  kufika  Kijijini hapo kwa lengo la kutoa elimu, baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nundu  wamesema kuwa, Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kujipambanua kwa kuendelea kuwajali Wananchi, kuwafuta machozi na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila Mtanzania bila kujali kipato cha chake. "Wakati mwingine katika kudai haki inaweza kufikia hatua unakua haujaridhika na haujui uende wapi...

MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAPOKEWA KWA KISHINDO LUDEWA

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Victoria Mwanziva akiongea na wananchi wa Ludewa alipowapokea wataalam wanaotekeleza Kampeni ya Mama Samia Wilayani humo. Mei 27, 2024. Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Athumani Msosole akitoa mada kwenye mkutano wa hadhara wilayani Ludewa katika kutekeleza Kampeni ya Mama Samia. Mei 27, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku & Athumani Msosole – WKS Ludewa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Compain - MSLAC) Mkoa wa Njombe umeambatana na zoezi la utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwenye kata na vijiji katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Njombe ikiwemo Wilaya ya Ludewa. Akiwapokea wataalam wanaounda timu ya msaada wa kisheria kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Victoria Mwanziva alisema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imefika wakati muafaka na wananchi wa Ludewa walikuwa wanaisubiri kwa hamu kutokana n...

ACHANENI NA MISIMAMO HASI – DC MAKETE

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Makete Bw. Juma Sweda akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ihela Kata ya Tandala katika kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Mei 28, 2024. Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Polisi Wilaya ya Makete Afande Nicholous Chilemile akitoa mada ya ukatili wa kijinsia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ihela Kata ya Tandala katika kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Mei 28, 2024. Afisa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. Henry Nyigu akitoa mada ya haki na wajibu wa mtoto kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihela, Mei 28, 2024 Kata ya Tandala. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Makete Mkuu wa Wilaya ya Makete Bw. Juma Sweda amewaasa wananchi kuacha misimamo hasi na kukubali ushauri wanaopewa na Wataalamu wanaotekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwani misimamo mingine inaenda kinyume na sheria na hivyo kuendelea kuchangia migogoro katika jamii. Mku...

MSLAC YALIFIKIA GEREZA LA NJOMBE

Image
  Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akipokea taarifa ya Gereza la Njombe. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Mary Makondo, Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu, Wataalamu na Wadau wa Sheria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Mkoani Njombe. Mei 27, 2024. Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwenye picha ya pamoja na  Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Mary Makondo, Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu, Wataalamu na Wadau wa Sheria mara baada ya kufika Gereza la Njombe kuzungumza na Wafungwa na Mahabusu  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Mkoani Njombe. Mei 27, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Hyasinta Kissima – WKS Njombe Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika maeneo ya vizu...

TATUENI KERO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI – DKT. KAZUNGU

Image
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiongea na wananchi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni ya MSLAC katika kijiji cha Mago Kata ya Lupalilo, Halmashauri ya Wilaya ya Makete. Mei 27, 2024. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiwazawadia baadhi ya akinamama wenye watoto wadogo waliohudhuria Mkutano wa Kampeni ya MSLAC katika kijiji cha Mago Kata ya Lupalilo, Halmashauri ya Wilaya ya Makete. Mei 27, 2024. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. William Makufwe (katikati) kwenye picha ya pamoja na timu inayotekeleza kampeni ya Mama Samia Wilayani humo. Mei 27, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Makete Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu amewataka Wataalam wanaotekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kutatua kero za kisheria wanazokabiliana nazo wananchi na zile watakazoshindwa kutatua kuziacha zimeandaliwa nyaraka kwenda ngazi za juu kwa aj...

MSLAC ITUMIKE KUTAFUTA SULUHU NA SIO MSHINDI

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Njombe, Mei 26, 2024. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akitoa salaam kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kuhutubia wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Njombe, Mei 26, 2024. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akitoa salaam wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Njombe, Mei 26, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akisalimiana na Wageni kutoka Wilaya ya Butiama waliofika mkoani Njombe kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Mkoani humo. Mei 26, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Hyasinta Kissima – WKS Njombe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko amewataka watoa huduma za Msaada wa Kish...

"TUWASAIDIE WANANCHI KUTATUA MIGORORO KUPITIA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA" – SAGINI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza   na washiriki wa mafunzo ya utoaji wa msaada wa kisheria (hawapo pichani) katika Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign, wakati aliposhiriki kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe Mei 25, 2024. Baadhi ya Wataalamu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa Msaada wa Kisheria katika Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe Mei 25, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwenye picha ya  pamoja na Wataalamu watakaoshiriki katika huduma za utoaji wa  msaada wa Kisheria katika Kampeni ya Mama Samia inayotarajiwa kuzinduliwa katika Mkoa wa Njombe Mei 26, 2024. Kushoto kwa kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima - WKS Njombe Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amew...

WANAFUNZI WAFANYA MJADALA JUU YA MSAADA WA KISHERIA

Image
  xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeyela iliyopo Mkoani Njombe Mjini leo 24 Mei, 2024 wameonesha umahiri wao katika kudadavua masuala mbalimbali walipokuwa wakifanya mjadala juu ya msaada wa kisheria huku mada ikisema "Je jamii inafahamu juu ya Msaada wa Kisheria?" Mjadala huu umeandaliwa na Timu ya Msaada wa kisheria kutoka katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayokusudiwa kuzinduliwa siku ya Jumapili tarehe 26 Mei, 2024 katika viwanja vya Stendi ya Zamani Njombe mjini.

BONANZA LA KUKATA NA SHOKA LARINDIMA VIWANJA VYA SABASABA NJOMBE

Image
 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe Bonanza kali la kukata na shoka limerindima leo katika viwanja vya Sabasaba Njombe mjini ambapo vijana wa Bodaboda wameminyana na vijana wa Bajaji huku Bajaji wakiibuka washindi kwa mikwaju ya penati ya 5 - 4 wakati huohuo Mashabiki wa Yanga wakipambana na mashabiki wa Simba huku mashabiki wa Simba wakiibuka na ushindi wa goli 2-1. Michezo hii ni shamra shamra za kuelekea uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign 26/05/2024 ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

KIPAUMBELE NI WILAYA AMBAZO HAZINA MAHAKAMA – SAGINI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akijibu maswali Bungeni, Mei 24, 2024, Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kipaumbele cha Serikali ni kujenga Mahakama kwenye Wilaya zote ambazo hazina Mahakama. Mhe. Sagini ameyasema hayo leo Mei 24, 2024 Bungeni Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mhe. Jonas Wiliam Mbunda Mbunge wa Mbinga Mjini aliyetaka kujua lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Mbinga. ”Kulingana na ukubwa wa changamoto tulizonazo za uhaba na uchakavu wa majengo, kwa sasa, kipaumbele ni kujenga majengo ya Mahakama katika Wilaya ambazo hazina kabisa majengo ya Mahakama.” Alisema. Mhe. Sagini amekiri kwamba jengo Mahakama ya Wilaya ya Mbinga   siyo la kisasa. Hata hivyo, jengo hilo bado lina hali nzuri kwa kuwa limekuwa likifanyiwa ukarabati mdogo mara kwa mara. Aidha, huduma za kimahakama zinatolewa bila changamoto katika jengo hilo a...

WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU DARMIKI WAFANYA ZIARA BUNGENI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Darmiki kilichopo Area A Jijini Dodoma walipotembelea Bunge kwa ziara ya mafunzo wakiwa wageni wake, Mei 24, 2024 Bungeni Dodoma. Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Darmiki kilichopo Area A Jijini Dodoma walipotembelea Bunge kwa ziara ya mafunzo wakiwa wageni wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini, Mei 24, 2024 Bungeni Dodoma. Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Darmiki kilichopo Area A Jijini Dodoma pamoja na wageni wengine wakipatiwa elimu kuhusu shughuli za Bunge walipotembelea Bunge kwa ziara ya mafunzo wakiwa wageni wa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini, Mei 24, 2024 Bungeni Dodoma.

SERIKALI KUENDELEA NA UTARATIBU WA PLEA BARGAINING – SAGINI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge, Mei 22, 2024 Bungeni Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema utaratibu wa kisheria wa Plea - Bargaining katika mashauri ya jinai umekuwa na faida nyingi na hivyo Serikali itaendelea kuutumia. Mhe. Sagini ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma Mei 22, 2024 alipokuwa anajibu swali la Mhe. Abubakar Damian Asenga (Kilombero) aliyetaka kujua kama Serikali inaona bado kuna umuhimu wa Sheria ya Plea - Bargaining . ”Tangu kuanza kwa utaratibu huu mwaka 2019 hadi Juni 2023 jumla ya mashauri 423 yamemalizika kwa utaratibu   Plea Bargaining ambayo yalihusisha watuhumiwa 1,040.   Kiasi cha Shilingi 54,643,730,080.13 zilirudishwa Serikalini kupitia utaratibu huu na shilingi 2,083,384,927.70 zilirudishwa kwa wahanga wa uhalifu. Kutokana na faida hizo, Serikali bado inaona umuhimu wa kuwa na utaratibu huu wa kish...

MUSWADA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA WAKAMILIKA – SAGINI

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge, Mei 22, 2024 Bungeni Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imekamilisha uandaaji wa muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kwamba taratibu zinaandaliwa za kuufikisha Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kisha kupitishwa kuwa sheria kamili. Mhe. Sagini ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma Mei 22, 2024 alipokuwa anajibu swali la Mhe. Dkt. Ntara Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua lini Serikali italeta Muswada wa Sheria ya Ndoa ili iendane sambasamba na vita dhidi ya ndoa za utotoni. “Wizara imekamilisha uandaaji wa Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa na hivi sasa muswada huo upo katika hatua za ndani za Serikali na mara hatua hizo zitakapokamilika muswada huo utawasilishwa Bungeni kwa utaratibu wa kawaida.” Alisema. Mhe. Sagini amesema Serikal...

SAGINI AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA TANZANIA

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiongea kwenye kikao alichoongoza kati ya Wizara, Taasisi zake  na Benki ya Dunia kupitia na kujadili mapendekezo ya mageuzi kwenye sekta ya sheria. Mei 22, 2024 Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Belete kwenye kikao kati ya Wizara, Taasisi zake  na Benki ya Dunia kupitia na kujadili mapendekezo ya mageuzi kwenye sekta ya sheria. Mei 22, 2024 Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiongoza kikao kati ya Wizara, Taasisi zake  na Benki ya Dunia kupitia na kujadili mapendekezo ya mageuzi kwenye sekta ya sheria. Mei 22, 2024 Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania Bw. Nathan Belete wakati wa kikao kati ya Wizara, Taasisi zake  na Benki ya Dunia kupitia na kujadili mapendekezo ya mageuzi...