ADHMA YETU NI KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI HAKI – DKT. PINDI CHANA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea wakati anafungua Mkutano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 11, 2024 Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati anafungua Mkutano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 11, 2024 Jijini Dodoma.Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisalimiana na baadhi ya Wabunge walioshiriki Mkutano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 11, 2024 Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiteta jambo na Wakili Onesmo Olengurumwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kabla ya kuanza Mkutano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 11, 2024 Jijini Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi
Dkt. Pindi Chana amesema nia ya Serikali iliyoko madarakani inayoongozwa na
Mhe. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona Wananchi
wanapata haki tena wanaipata kwa wakati. Katika kutimiza adhma hiyo
Serikali imeendelea kuboresha utoaji haki, kuwa na Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora na kuwa na Tume ya Haki Jinai.
Dkt.
Chana ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano ulioandaliwa na Mtandao wa Watetezi
wa Haki za Binadamu kwa lengo la kujadili kwa pamoja masuala yanayogusa haki za
binadamu, Mei 11, 2024 Jijini Dodoma.
Aidha,
amesema Serikali itaendelea kutekeleza mikataba ya Kikanda na Kimataifa ya haki
za binadamu, kuendelea kutoa elimu ya haki binadamu, wakati wote kuwa na sera
za kutetea haki za binadamu na kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa haki za
binadamu.
Akiongelea
ushirikiano na Watetezi wa hakli za Binadamu, Dkt. Chana amesema Serikali itaendelea
kufanya kazi kwa pamoja na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu kwa lengo
moja la kuona Tanzania inaendelea kuwa na amani.
Comments
Post a Comment