BONANZA LA KUKATA NA SHOKA LARINDIMA VIWANJA VYA SABASABA NJOMBE
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe
Bonanza kali la kukata na
shoka limerindima leo katika viwanja vya Sabasaba Njombe mjini ambapo vijana wa
Bodaboda wameminyana na vijana wa Bajaji huku Bajaji wakiibuka washindi kwa
mikwaju ya penati ya 5 - 4 wakati huohuo Mashabiki wa Yanga wakipambana na
mashabiki wa Simba huku mashabiki wa Simba wakiibuka na ushindi wa goli 2-1.
Michezo hii ni shamra shamra za kuelekea uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid
Campaign 26/05/2024 ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Comments
Post a Comment