CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 62
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao alipokutana na Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mhe. David Kihenzile leo tarehe
10 Mei, 2024 ofisi za Bunge Dodoma.
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.
Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Rais
wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mhe. David Kihenzile leo tarehe 10 Mei,
2024 ofisi za Bunge Dodoma. Kikao hicho kilihusu maandalizi ya Maadhimisho ya
miaka 62 ya Chama hicho nchini Tanzania yatakayofanyika Mei 11, 2024 Ukumbi wa Jakaya
Kikwete Jijini Dodoma. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu.
Comments
Post a Comment