CHANA ATEMBELEA MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ARUSHA
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akisalimiana na Rais wa
Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jaji Nesto Kayobera, Mei 02, 2024 Jijini
Arusha.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi
Dkt. Pindi Chana akiwa na Jaji Imani Aboud, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki
za Binadamu na Watu, Mei 02, 2024 Jijini Arusha.
Rais
wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jaji Nesto Kayobera (katikati),
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.
Mary Makondo, Mei 02, 2024 Jijini
Arusha.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria alioambatana nao alipotembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kulia kwake ni Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jaji Nesto Kayobera na kulia kabisa ni Katibu Mkuu Bi. Mary Makondo, Mei 02, 2024 Jijini Arusha.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Lusajo Mwakabuku - WKS
Arusha
Waziri
wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana leo, Alhamisi Mei 02.2024
ametembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopo jijini
Arusha, ambapo akiwa hapo amepokelewa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Nesto
Kayobera
Akizungumza
kwenye viunga vya Mahakama hiyo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema katika
mazungumzo yao wawili hao wamekubaliana kushirikiana kwenye nyanja mbalimbali
ikiwemo Majaji wa Mahakama hiyo kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma Chuo cha
Sheria hapa nchini (Law School of Tanzania), sambamba na Chuo cha Uongozi wa
Mahakama kilichopo Lushoto, mkoani Tanga ambapo imeelezwa kuwa hivi karibuni
maafisa wa Mahakama hiyo walitembelea chuoni hapo kwa ajili ya kutoa mafunzo
kwa Majaji na Mahakimu
Aidha,
amesema wamekubaliana kuwa Mawaziri wanaohusika na masuala ya Katiba na Sheria
kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutengeneza utaratibu wa
kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kujadili maboresho ya sheria
mbalimbali na kuzifahamu sheria hizo
Kwa
upande wake Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jaji Nesto Kayobera
licha ya kumshukuru Waziri kwa kutembelea kwenye Mahakama hiyo, lakini pia
amesema yeye binafsi (Jaji Kayobera) alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan siku za nyuma ambapo Rais Dkt. Samia
alisema Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Mahakama hivyo kutoa wito kwa
Mahakama hiyo kutekeleza shughuli zake kwa
uhuru na uwazi
Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara ya Katiba na Sheria inaendelea kutekeleza falsafa ya '4R' iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho ya masuala mbalimbali kwenye taasisi zote zilizopo chini yake.
Comments
Post a Comment