DKT. CHANA ATEMBELEA CHUO CHA UANASHERIA KWA VITENDO
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana akiongea
alipofanya kikao na Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo,
Mei 18, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Prof.
Sist J. Mramba akiongea kwenye kikao cha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi
Dkt. Pindi Hazara Chana na Uongozi wa Taasisi hiyo, Mei 18, 2024 Jijini Dar es
Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara
Chana leo Mei 18, 2024 Jijini Dar es Salaaam amefanya kikao na Uongozi wa
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
(Law School of Tanzania) ukiongozwa Prof. Sist J. Mramba Kaimu Mkuu wa
Taasisi hiyo ili kujadili kanuni na
taratibu mbalimbali za uendeshaji Taasisi na kuona namna ya kuboresha kanuni hizo ili kukuza ufanisi
katika mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo.
Comments
Post a Comment