"JAMII INAHITAJI ELIMU ZAIDI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA" WAZIRI DKT. PINDI CHANA
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimsikiliza Wakili Onesmo Olengurumwa
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 07, ofisi za
Bunge Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongoza kikao alipokutana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 07, ofisi za Bunge Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja baada
ya kufanya kikao na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Mei 07, ofisi za
Bunge Dodoma.
xxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi amesema hayo
wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Wakili Onesmo
Olengurumwa ambaye ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za
Binadamu - Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) kikao kilichofanyika
Mei 7,2024 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma .
Akizungumza
katika kikao hicho kilichowahusisha Wataalamu kutoka ofisi hizo mbili, Waziri
Chana amesema jitihada zaidi inahitajika katika kuongeza kasi ya utoaji
wa elimu kwa jamii ili kupinga matukio ya ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia.
"Elimu
ya ukatili wa kijinsia inapotolewa mapema kwa watoto huwasaidia kutambua haki
zao na kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ukatili huo” alisema Mhe. Dkt.
Chana
Katika
kikao hicho, makubaliano mengine yaliyoafikiwa ni pamoja na kuwepo na mpango wa
kuendelea na utoaji wa elimu kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya athari
za uvunjaji wa sheria, kupinga ukatili wa kijinsia ukienda sambamba na utoaji
elimu kwa watoto wa shule za msingi na kusisitiza kuwa Wizara yake
itabainisha maeneo ambayo yanahitaji kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo
THRDC katika kuendeleza jitihada za kutetea haki za binadamu.
Katika
hatua nyingine kikao hicho pia kilijadiliana kuhusu kukamilika kwa Mpango
kazi wa Kitaifa wa Pili wa Haki za Binadamu, Ushiriki wa Serikali katika mifumo
ya haki za binadamu ya Kikanda na Kimataifa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha
taarifa za utekelezaji wa mikataba husika ambayo nchi imeridhia.
Comments
Post a Comment