KIPAUMBELE NI WILAYA AMBAZO HAZINA MAHAKAMA – SAGINI
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akijibu maswali Bungeni, Mei 24, 2024, Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi –
WKS Dodoma
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kipaumbele cha Serikali ni kujenga Mahakama
kwenye Wilaya zote ambazo hazina Mahakama.
Mhe. Sagini ameyasema hayo
leo Mei 24, 2024 Bungeni Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mhe. Jonas Wiliam Mbunda Mbunge wa Mbinga Mjini aliyetaka
kujua lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya
Mbinga.
”Kulingana na ukubwa wa
changamoto tulizonazo za uhaba na uchakavu wa majengo, kwa sasa, kipaumbele ni
kujenga majengo ya Mahakama katika Wilaya ambazo hazina kabisa majengo ya
Mahakama.” Alisema.
Mhe.
Sagini amekiri kwamba jengo Mahakama ya Wilaya ya Mbinga siyo la kisasa. Hata hivyo, jengo hilo bado
lina hali nzuri kwa kuwa limekuwa likifanyiwa ukarabati mdogo mara kwa mara.
Aidha, huduma za kimahakama zinatolewa bila changamoto katika jengo hilo ambalo
limeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwezesha utoaji wa huduma
kupitia mifumo ya kielektroniki inayotumiwa na Mahakama ikiwemo uendeshaji wa
mashauri.
Comments
Post a Comment