MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAPOKEWA KWA KISHINDO LUDEWA
Na Lusajo Mwakabuku & Athumani Msosole –
WKS Ludewa
Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada
wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Compain - MSLAC) Mkoa wa Njombe
umeambatana na zoezi la utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwenye kata na
vijiji katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Njombe ikiwemo Wilaya ya Ludewa.
Akiwapokea wataalam wanaounda
timu ya msaada wa kisheria kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi,
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi. Victoria Mwanziva alisema Kampeni ya Msaada wa
Kisheria ya Mama Samia imefika wakati muafaka na wananchi wa Ludewa walikuwa
wanaisubiri kwa hamu kutokana na migogoro mbalimbali inayohusu masuala ya
kisheria inayowakumba wananchi wake.
“Sisi wana Ludewa tunamshukuru
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Kampeni hii ya Kitaifa, Wataalam
wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wapo Ludewa na sisi Wilaya ya
Ludewa tumeipokea kampeni hii kwa mikono miwili na kazi inaendelea wilayani
hapa” Alisema DC Mwanziva.
Aidha mara baada ya timu kuwasili wilayani na
kujitambulisha katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, timu ya wataalam wakiongozwa na
Mkuu wa Wilaya Bi. Manziva walielekea katika kituo cha Radio kilichopo Ludewa
mjini (Rafiki FM) na kuelezea kuhusu ujio wa Mama Samia Legal Aid Campaign
wilayani humo kabla ya kuendelea kutoa Elimu mashuleni na mikutano wa hadhara
kwa lengo la kuelimisha jamii na kusikiliza changamoto mbalimbali za Kisheria
na kuzipatia ufumbuzi.
Comments
Post a Comment