MAWAKILI WA SERIKALI TUISHAURI IPASAVYO SERIKALI
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Jumanne Sagini akizungumza na Mawakili wa
Serikali (hawapo pichani) katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya
uendeshaji wa mashauri ya Serikali Mei 20, 2024 katika ukumbi wa Lush Garden
jijini Arusha.
Wakili
Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akizungumza katika ufunguzi wa
mafunzo ya Mawakili wa Serikali Jijini Arusha ambapo amesema mafunzo hayo
yatahusisha pia tathmini ya namna Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali zimefanikisha kuratibu na
kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi nje na ndani ya nchi.
Naibu
Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya Serikali yanayofanyika kwa muda wa siku
tatu kuanzia Mei 20-22, 2024 Lush garden jijini Arusha.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akiongoza zoezi la
uzinduzi wa nembo ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Kulia kwa Naibu
Waziri ni Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, akifuatiwa na
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (aliyeketi katikati ) akiwa
katika picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka Wizara mbalimbali mara
baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali Mei 20, 2024 Lush
Garden jijini Arusha.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Hyasinta Kissima-WKS Arusha
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewataka Mawakili wa
Serikali kuishauri ipasavyo Serikali na Taasisi zake wakiwemo Viongozi kuhusu
namna ya kushughulikia na kumaliza migogoro na Wananchi au Wawekezaji bila
kuathiri maslahi ya Nchi.
Mhe.
Sagini ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili wa Serikali
yanayofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Mei 20, 2024, Lush Hotel
Jijini Arusha.
"Kwenye
eneo hili napenda kuwashauri kuwa more 'proactive rather than reactive'
mtakapoona Viongozi wetu katika utendaji wao kuna dalili ya kuleta migogoro
kwenye utekelezaji wa mikataba, msisubiri mambo yaharibike. Ninyi Mawakili wa
Serikali mpo, mkisubiri yakaharibika watu wakaenda kwenye vyombo vya kutoa haki
kama Mahakama au Mabaraza ya Usuluhishi ya ndani na nje ya nchi
maana yake kazi imeanza kuwa ngumu. Lakini kama tungewahi tukatoa ushauri
mapema tungezuia hali isiwe mbaya." Alisema Naibu Waziri Sagini
Aidha,
ameipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa mafanikio makubwa
ikiwemo kuitetea Serikali katika mashauri ya madai na usuluhishi jambo ambalo
limepelekea kuokoa fedha nyingi za Serikali katika kipindi kifupi tangu
kuanzishwa kwa ofisi.
Aliendelea
kusema, matumaini ya Wizara ya Katiba na Sheria ni Mawakili hao kuendelea
kuyatumia mafunzo hayo kama chachu katika kuendeleza mafanikio hayo
na kuwafanya kutoridhika bali kuamsha ari mpya katika kuyaishi na kuyaendeleza
kwa faida ya Serikali, Nchi na Wanachi.
Wakili
Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende aliainisha ajenda kuu tatu katika
mafunzo hayo ambapo ajenda ya kwanza ikiwa ni uzinduzi wa nembo ya Ofisi ya
Wakili Mkuu wa Serikali ambayo itatumika kama utambulisho katika mawasiliano
mbalimbali, ajenda ya pili ikihusisha mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yanayohusu
uwasilishaji wa mada mbalimbali na majadiliano na ajenda ya tatu ikiwa ni
kufanya tathmini ya namna ambavyo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa
kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali zimefanikisha kuendesha na
kuratibu uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi nje na ndani ya nchi.
Ofisi
ya Wakili Mkuu wa Serikali tangu mwaka 2020 imekuwa na utaratibu wa kuandaa
mafunzo kwa Mawakili wa Serikali ili kuongeza maarifa na ujuzi zaidi
katika maeneo mtambuka ambayo Mawakili hujishughulisha nayo ili kuongeza
ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa weledi mkubwa
ambapo kwa mwaka 2024, jumla ya Mawakili 500 kutoka Wizara zote Nchini,Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar,
Taasisi za Umma, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Taifa, Wakala wa Serikali,
Mashirika ya Umma, Mamlaka za Udhibiti na Vyuo mbalimbali hapa Nchini
wameshiriki.
Comments
Post a Comment