MSLAC YALIFIKIA GEREZA LA NJOMBE
Naibu Waziri Wizara ya Katiba
na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akipokea
taarifa ya Gereza la Njombe. Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa
Wizara Bi. Mary Makondo, Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu, Wataalamu
na Wadau wa Sheria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa
Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Mkoani Njombe. Mei 27, 2024.
Naibu
Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwenye picha ya pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Mary
Makondo, Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu, Wataalamu na Wadau
wa Sheria mara baada ya kufika Gereza la Njombe kuzungumza na Wafungwa na
Mahabusu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria
ya Mama Samia (MSLAC) Mkoani Njombe. Mei 27, 2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Hyasinta Kissima – WKS Njombe
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama
Samia katika maeneo ya vizuizi ikiwemo Magereza imelenga kutimiza dhamira ya
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuona haki inatendeka kwa Watanzania wote
na kwa wakati.
Mhe. Sagini ameyasema hayo Mei
27, 2024 wakati alipotembelea Gereza ya Njombe akiwa ameambatana na Katibu Mkuu
wa Wizara Bi. Mary Makondo, Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Sylvester
Mwakitalu, Wataalamu na Wadau wa Sheria ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Njombe.
"Yapo maeneo mbalimbali
ambayo Kampeni hii imelenga kuyafikia ikiwemo Magereza ili kukabiliana na
mapungufu yanayoweza kuwa yamejitokeza katika usimamizi wa
Sheria.Wafungwa na Mahabusu tulionao wanategemea washauriwe ipasavyo. Katika
maeneo walipokwama na wengine mpaka wanahukumiwa msamaha wa Mhe. Rais unatoka
lakini jamii haiwataki kuwapokea.Tunatengeneza mazingira gani ya usuluhishi
lakini hata katika mazingira ya kudhaminiwa hata katika dhamana zilizo wazi
Wananchi hawapo tayari kuwadhamini tunafanya nini ili wawe raia
wazuri."Alisema Naibu Waziri Sagini.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na Sheria Bi. Mary Makondo amesema kuwa Wizara kupitia mradi wa e-justice
itawezesha upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya mifumo ya kimtandao katika
Mahakama, Magereza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Tume ya kurekebisha Sheria na wadau
wengine kadri fedha zitakapokuwa zinapatikana.
Ikumbukwe kuw, tangu
kuzinduliwa kwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Njombe Mei
26, 2024 timu za Wataalamu wa Sheria zinaendelea kutoa elimu na kutatua
changamoto za Kisheria walizokuwa wanakabiliana nazo Wananchi katika Halmashauri
zote sita za mkoa wa Njombe na kuendelea kuwafikia katika maeneo ya
Magereza ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kila Mtanzania.
Comments
Post a Comment