MUSWADA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA WAKAMILIKA – SAGINI
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria
imekamilisha uandaaji wa muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kwamba taratibu
zinaandaliwa za kuufikisha Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kisha kupitishwa
kuwa sheria kamili.
Mhe. Sagini ameyasema hayo
Bungeni Jijini Dodoma Mei 22, 2024 alipokuwa anajibu swali la Mhe. Dkt. Ntara Mbunge
wa Viti Maalum aliyetaka kujua lini Serikali italeta Muswada wa Sheria ya Ndoa ili
iendane sambasamba na vita dhidi ya ndoa za utotoni.
“Wizara imekamilisha uandaaji
wa Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa na hivi sasa muswada huo upo katika
hatua za ndani za Serikali na mara hatua hizo zitakapokamilika muswada huo
utawasilishwa Bungeni kwa utaratibu wa kawaida.” Alisema.
Mhe. Sagini amesema Serikali
ilianza maadalizi muswada huo baada ya kukusanya maoni ya Wadau mbalimbali
wakiwemo Wazee wa kimila, Viongozi wa kidini, Wanataaluma, Wanafunzi wa ngazi
mbalimbali, Watu mashuhuri na Waheshimiwa Wabunge juu ya maboresho ya sheria
hiyo kuhusu kuondoa mabishano ya umri upi kwa sasa uwe wa kuoa au kuolewa.
Comments
Post a Comment