SAGINI AKUTANA NA WATUMISHI WA VITENGO VYA TEHAMA NA MAWASILIANO SERIKALINI
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini amekutana na kufanya mazungumzo na Watumishi wa
Vitengo vya TEHAMA na Mawasiliano Serikalini kwa lengo la kujua majukumu yao,
utekelezaji wa majukumu yao na changamoto katika kutimiza kazi zao. Katika kikao
hicho ambacho kilikuwa cha mwisho katika utaratibu aliokuwa amejiwekea kukutana
na Idara na Vitengo ili kujua shughuli za Wizara amesisitiza ushirikiano, umoja
na mawasiliano mazuri kati ya watumishi na Viongozi wao. Mei 16, 2024 Mtumba.
Comments
Post a Comment