TATUENI KERO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI – DKT. KAZUNGU
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akiwazawadia baadhi
ya akinamama wenye watoto wadogo waliohudhuria Mkutano wa Kampeni ya MSLAC
katika kijiji cha Mago Kata ya Lupalilo, Halmashauri ya Wilaya ya Makete. Mei
27, 2024.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. William Makufwe (katikati) kwenye picha
ya pamoja na timu inayotekeleza kampeni ya Mama Samia Wilayani humo. Mei 27,
2024.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS
Makete
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu amewataka Wataalam
wanaotekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kutatua kero
za kisheria wanazokabiliana nazo wananchi na zile watakazoshindwa kutatua
kuziacha zimeandaliwa nyaraka kwenda ngazi za juu kwa ajili ya kutatuliwa.
Dkt.
Kazungu ameyasema hayo Mei 27, 2024 alipotembelea Timu inayotekeleza Kampeni ya
Mama Samia katika Halmashauri ya Makete ambayo ilikuwa ikifanya mkutano na
wananchi wa Kijiji cha Mago Kata ya Lupalilo.
”Tatueni
changamoto za kisheria wanazokabiliana nazo wananchi hawa na kero
zitakazowashinda kutokana na muda hakikisheni mnawaandalia nyaraka za kisheria
ili waende ngazi zingine,” alisema.
Dkt.
Kazungu aliwashukuru wananchi waliojitokeza kwenye kampeni hiyo na kutumia
wasaa huo kuwazawadia pesa akina mama waliofika kwenye mkutano wakiwa na watoto
wadogo.
Kabla
ya kuanza kutekeleza kampeni Wilayani humo timu hiyo iliripoti ofisi ya Mkuu wa
Wilaya na kuongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makete Bw. William Makufwe
ambaye amewataka watekelezaji wa kampeni hiyo kutumia lugha inayoeleweka,
"tumieni lugha nyepesi wakati mnatekeleza kampeni hiyo muhimu ya kutoa
uelewa wa sheria ili Wananchi wawaelewe, lakini pia niwaombe kuangalia
uwezekano wa kubadili ratiba yenu kwa kuongeza idadi ya vijiji kwa kuzingatia
kwamba wananchi wetu ni wachache na baadhi ya vijiji viko karibu karibu."
Akifafanua
juu ya fidia ya maeneo ya miradi, Bw. Advent Tweve, Afisa Ardhi Halmashauri ya
Wilaya ya Makete amesema pale ambapo mradi umeombwa au kuibuliwa na kijiji ni
wajibu wa kijiji kutoa eneo la mradi bure
isipokuwa pale ambapo Serikali imeleta mradi na kupelekea uhitaji wa
eneo, Serikali huwajibika kutoa fidia.
“Mnapoibua
Miradi nakuhitaji eneo la mwanakijiji mwenzenu hakikisheni mnamwelewesha
umuhimu wa mradi huo ili atoe eneo bure kwa hiari yake, tena mhakikishe
mmeandikishana ili kuepuka migogoro hapo baadaye.” Alisema Bw. Tweve.
Comments
Post a Comment