TUME YA KUREKEBISHA SHERIA JITANGAZENI WADAU WA SHERIA WAWATAMBUE - N/W SAGINI
Na Yasinta Kissima – WKS Dodoma
Akizungumza
mara baada ya kutembelea Makao Makuu ya Tume ya Kurekebisha Sheria na Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora jijini Dodoma, Mei 8, 2024 Naibu Waziri wa Katiba
na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameitaka Tume ya Kurekebisha Sheria kujitangaza
na kutoa elimu kwa Wadau wa Sheria ili Tume iweze kushiriki ipasavyo
katika kufanya mapitio ya Sheria mbalimbali.
Mhe. Sagini amesema kuwa ipo
changamoto ya baadhi ya Wadau wa Sheria kutokujua vizuri majukumu ya Tume na
hivyo kuchelewa kuishirikisha Tume katika kufanya mapitio ya Sheria zao.
"Tume ipo kwa mujibu wa
Sheria na Katiba yetu na inawajibu wa kufanya tathmini ya Sheria zilizopo kuona
zile zilizopitwa na wakati, zinazohitaji marekebisho, utekelezaji wake na
changamoto ili kuishauri Serikali namna bora ya kuboresha Sheria hizo." Alisema
Naibu Waziri Sagini.
Kuhusu utekelezaji wa miradi
ya Maendeleo, Mhe. sagini amesema kuwa mpaka sasa Wizara kwa kushirikiana na
Taasisi zilizopo chini yake imeanza kuandika maandiko mbalimbali ili kuweza
kuvutia fedha kutoka Serikali au Wadau mbalimbali wa Maendeleo na ameitaka Tume
ya Kurekebisha Sheria kushiriki ipasavyo na kutoa mapendekezo yao katika miradi
itakayopendekezwa.
Comments
Post a Comment