TUMEJIPANGA - MTAKA & CHANA
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na
Wahabari kuhusu kufanyika kwa Kampeni ya Mama Samia mkoaji Njombe. Mei 22, 2024
Njombe. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka.
Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka kwa
pamoja wamesema wamejiandaa kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa
Tanzania wananufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria maarufu kama "Mama
Samia Legal Aid Campaign"
Viongozi hao wameyasema hayo
Mei 22, 2024 walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe juu ya
uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani humo.
Utekelezaji wa Kampeni hiyo
ulianzia jijini Dodoma ambapo
ilizinduliwa tarehe 27 Aprili, 2023, na Zanzibar tarehe 9 Mei, 2023.
Kwa sasa Kampeni hii imeufikia
Mkoa wa Njombe ambapo huduma za msaada wa kisheria zitatolewa bure kwa Wananchi
katika Halmashauri zote sita kuanzia tarehe 26 Mei, 2024.
Comments
Post a Comment