"TUWASAIDIE WANANCHI KUTATUA MIGORORO KUPITIA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA" – SAGINI
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini akizungumza
na washiriki wa mafunzo ya utoaji wa msaada wa kisheria (hawapo pichani)
katika Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign, wakati aliposhiriki kwenye
uzinduzi wa mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya
Mji Njombe Mei 25, 2024.
Baadhi ya Wataalamu walioshiriki
mafunzo ya utoaji wa Msaada wa Kisheria katika Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign,
katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe Mei 25, 2024.
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini kwenye picha ya
pamoja na Wataalamu watakaoshiriki katika huduma za utoaji wa msaada wa Kisheria katika Kampeni ya Mama
Samia inayotarajiwa kuzinduliwa katika Mkoa wa Njombe Mei 26, 2024. Kushoto kwa
kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Hyasinta Kissima - WKS Njombe
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewataka Wataalamu watakaoshiriki katika zoezi la
utoaji msaada wa kisheria katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia
"Mama Samia Legal Aid Campaign" kuhakikisha wanatoa elimu kikamilifu
ili kutatua migogoro na kero za Wananchi.
Mhe. Sagini ameyasema hayo
Mei 25, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakati akifungua
mafunzo ya siku moja kwa Wataalamu watakaoshiriki katika zoezi la kutoa
msaada wa Kisheria kwa muda wa siku kumi katika Halmashauri sita za Mkoa wa
Njombe.
"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanzisha Kampeni ya Msaada
wa Kisheria ya Mama Samia ili kuhakikisha kuwa kila Mwananchi ambaye hana uwezo
wa kuwafikia Mawakili na Wanasheria kunufaika na huduma hii. Kampeni hii imekua
na manufaa makubwa sana kwa Wananchi. Ninaamini ninyi mlioaminiwa kufanya kazi
hii mtathamini uzito huu ambao Mhe. Rais ameuweka kupitia kampeni hii."
Alisema Mhe. Sagini.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Sagini ameelekeza ni vyema Wizara ya Katiba na Sheria ikaona umuhimu wa
kufanya tafiti mbalimbali ili kuona madhara yatokanayo na watu kushindwa
kufahamu haki zao Kisheria ambapo wakati mwingine malalamiko hayo huenda yakasababishwa
na Watumishi wa Umma wasiotimiza wajibu wao ipasavyo.
Tangu kuzinduliwa kwa Kampeni
hiyo Kitaifa, Njombe ni Mkoa wa saba utakaoenda kunufaika na msaada huo wa
Kisheria, na jumla ya Wataalamu 86 wamepatiwa mafunzo hayo watakaotoa msaada
huo katika Halmashauri sita za Mkoa wa Njombe.
Comments
Post a Comment