WANAFUNZI WAFANYA MJADALA JUU YA MSAADA WA KISHERIA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe
Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Mbeyela iliyopo Mkoani Njombe Mjini leo 24 Mei, 2024 wameonesha
umahiri wao katika kudadavua masuala mbalimbali walipokuwa wakifanya mjadala
juu ya msaada wa kisheria huku mada ikisema "Je jamii inafahamu juu ya
Msaada wa Kisheria?" Mjadala huu umeandaliwa na Timu ya Msaada wa kisheria
kutoka katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayokusudiwa kuzinduliwa siku ya
Jumapili tarehe 26 Mei, 2024 katika viwanja vya Stendi ya
Zamani Njombe mjini.
Comments
Post a Comment