WANANCHI LUPILA WAITWISHA MSLAC KERO YA WANYAMA WAHARIBIFU
Afisa
Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Bw. Francis Malembo akitoa
mada ya wanyamapori na makatazo kwenye Hifadhi za Taifa na Mapori Tengefu
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila
Mei 30, 2024 Makete.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
William Mabusi – WKS
Makete
Wananchi
wa Kijiji cha Lupila katika Kata ya Lupila Wilayani Makete wameitwisha Timu
inayotekeleza Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Wilayani
humo kero ya wanyama nyani na ngedere ambao wamekuwa tishio kwa kuharibu mazao
na kutishia amani.
Malalamiko
hayo yametolewa na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini
hapo Mei 30, 2024 ikiwa ni katika kutekeleza kampeni hiyo.
Bw.
Naftali Ilomo mkazi wa kijiji cha Lupila wa kitongoji cha Upakilwa akitoa kero
yake amesema, “Serikali ifanye utaratibu wa kuwafukuza nyani na ngedere maana wamekuwa
kero karibu kwenye vijiji vyote vya Wilaya ya Makete iwe mvua iwe kiangazi,
Wazazi wamekuwa wakihatarisha usalama wa watoto kwa kuwaacha majumbani kwenda
kuhamia nyani na ngedere.”
Kilio
kama hicho kilitolewa na wakazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama ambao
wameomba Serikali iwakusanye na kuwapeleka wanyama hao kwenye hifadhi ama sivyo
waruhusiwe kuwaua.
Akitoa
mada ya wanyamapori na makatazo kwenye Hifadhi za Taifa na Mapori Tengefu Afisa
Wanyamapori Bw. Francis Malembo kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori –
TAWA amesema ni kinyume cha sheria kuuwa wanyamapori bila kibali, kwa kufanya
hivyo ni kuingia kwenye mgogoro na Serikali na ndiyo umuhimu wa kampeni hiyo
kutoa elimu kwa wananchi kuepusha migogoro.
“Mnapobaini
wanyamapori kwenye maeneo yemu toeni taarifa kwa viongozi ambao nao watatoa
taarifa kwa Afisa Wanyamapori wa Wilaya ili hatua stahiki zichukuliwe.” Alisema
Bw. Malembo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bw. William Makufwe
alikiri kuwepo kwa changamoto ya ngedere kwenye maeneo mengi Wilayani humo na
kwamba unaandaliwa utaratibu wa kuwafukuza na pale ambapo watakuwa wamezidi upo
utaratibu wa kuwauwa lakini kwa malekezo maalum kutoka mamlaka husika.
Akihitimisha
mada yake Bw. Malembo aligusia makatazo kwenye hifadhi za Taifa kuwa ni pamoja
na mwananchi haruhusiwi kuingia kwenye hifadhi bila kibali, hairuhusiwi kufanya
shughuli yoyote ya kijamii kama kukata kuni, kuingiza mifugo, kulima au kuwinda
bila kibali.
Comments
Post a Comment