WIZARA ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA II – DKT. CHANA
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasili viwanja vya
Chinangali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia na Uzinduzi wa Mpango Kazi wa
Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili, Mei 15,
2024 Jijini Dodoma. Kulia ni Bi. Ester Msambazi Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria
aliyemwakilisha Katibu Mkuu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na William Mabusi – WKS
Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara yake itaendelea
kushirikiana na Wizara za Kisekta, Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wadau
wa Maendeleo na wananchi katika kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 –
2028/29) kuhakikisa kwamba haki kwa wanawake na watoto inapatikana kwa wakati
na kwa ufanisi kupitia huduma ya msaada wa kisheria.
Dkt.
Pindi ameyasema hayo alipokuwa akitoa salaam na tamko la Wizara kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Familia na Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili
dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili, Mei 15, 2024 Jijini Dodoma.
“Wizara
itaendelea kutoa huduma ya msada wa kisheria, kuweka mazingira wezeshi ya
upatikanaji haki, kufanya mapitio ya sheria kubainisha maeneo yanayohitaji
kufanyiwa marekebisho, kuweka sera na kanuni zinatoa ulinzi kwa wanawake na
watoto ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na makundi maalumu.”
Amesema Dkt. Pindi.
Aidha,
Dkt. Pindi amesema Wizara itaendelea kuratibu na kutekeleza mapendekezo ya Tume
ya kuangalia jinsi ya kuimarisdha Taasisi za haki jina nchini, Kuwajengea uwezo
watekelezaji wa sheria ili waweze kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na
watoto, Kuendelea kuratibu na kutekeleza Kampeni ya Kisheria ya Mama Samia
katika mikoa yote nchini.
Comments
Post a Comment