Posts

Showing posts from June, 2024

RAIS TLS AISHAURI WIZARA KUJIKITA KWENYE MAGEUZI YA HAKI JINAI

Image
  Mtaalam Mshauri wa mradi wa Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika Kupambana na Rushwa Nchini – BSAAT na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Harlod Sungusia akitoa mada ya utekelezaji wa Mradi wa BSAAT na Upimaji Matokeo ya Mradi huo. Juni 29, 2024 mjini Morogoro. Kikao Kazi cha kufanya Tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24 na kuandaa Mpango Kazi wa mradi kwa mwaka 2024/25. Juni 29, 2024 mjini Morogoro. Bw. Oswin Mkinga mmoja wa washiriki wa Kikao Kazi cha kufanya Tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24 na kuandaa Mpango Kazi wa mradi kwa mwaka 2024/25 akichangia hoja. Juni 29, 2024 mjini Morogoro. Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo akifafanua jambo kwenye Kikao Kazi cha kuandaa Andiko la Kuanzisha Mfuko wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi. Juni 29, 2024 mjini Morogoro. Sehemu ya washiriki kwenye Kikao Kazi cha kuandaa Andiko

MRADI WA BSAAT NA UBORESHAJI WA MFUMO WA HAKI JINAI NCHINI

Image
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo akitoa tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24, tarehe 28 Juni, 2024 mjini Morogoro. Mchumi Mwandamizi na Afisa Kiungo Mradi wa BSAAT kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Elilanga Kaaya akitoa mada kwenye kikao cha tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24, tarehe 28 Juni, 2024 mjini Morogoro. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WKS Morogoro Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo amesema Wizara imeendelea kunufaika na Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika Kupambana na Rushwa Nchini (Building Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania - BSAAT) kwa kutekeleza majukumu mbalimbali yanayohusu kuboresha mfumo wa haki jinai nchini. Bi. Mpembo amesema hayo kwenye kikao cha tathmini ya mradi huo kwa kazi zilizofanywa kwa mwaka 2023/24, tarehe 28 Juni, 2024

DKT. GWAJIMA AONGOZA MKUTANO WA JUKWAA LA HAKI JINAI KAMATI YA MAWAZIRI

Image
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiongoza Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri kama Mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika Juni 27, 2024 Kumbi za Bunge Jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini akichangia mada kwenye Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri uliofanyika Juni 27, 2024 Kumbi za Bunge Jijini Dodoma. Sehemu ya washiriki kwenye Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri uliofanyika Juni 27, 2024 Kumbi za Bunge Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameongoza Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri kwa leo kama Mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika Juni 27, 2024 Kumbi za Bunge Jijini Dodoma. Katika Mkutano huo uliotanguliwa na Kikao cha Makatibu Wakuu, pamoja na mambo mengine wamejadili utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya

PINDI CHANA AFUNGUA MAFUNZO YA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia kwenye Kikao Kazi cha Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Matukio Muhimu ya Kibinadamu, Juni 27, 2024 Njombe. Afisa Mtendaji Mkuu na Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Bw. Frank K. Frank akitoa taarifa ya utangulizi kwenye Kikao Kazi cha Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Matukio Muhimu ya Kibinadamu, Juni 27, 2024 Njombe. Baadhi ya Washiriki kwenye Kikao Kazi cha Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Matukio Muhimu ya Kibinadamu, Juni 27, 2024 Njombe. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Mwandishi Wetu - Njombe Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 27, 2024 amefungua mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Udhamini yaliofanyika katika ukumbi wa Agreement  mkoani Njombe. Mhe. Pindi Chana akifungua mafunzo hayo amesisitiza juu ya umuhimu wa Usajili wa matukio

KUNA SULUHISHO LA KERO ZENU NDANI YA SERIKALI – MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Image
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akihutubia alipokuwa anazindua Kliniki ya sheria, Juni 26, 2024 Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dodoma. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akitoa salaam kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzindua Kliniki ya sheria, Juni 26, 2024 Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wataafu Tanzania wanaolipwa na Hazina mzee John Joseph Kanyeto akitoa kero yake kabla ya kuzindua Kliniki ya sheria, Juni 26, 2024 Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dodoma. Meza Kuu kwenye picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya uzinduzi wa Kliniki ya sheria, Juni 26, 2024 Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WKS Dodoma Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewahakikishia wananchi kuwa Serik

TAKWIMU ZA MATUKIO MUHIMU YA KIBINADAMU ZIBORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati wa kufungua Kikao Kazi cha kutathmini hali ya Utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano na kuzindua Taarifa ya kitakwimu ya usajili wa matukio muhimu ya kibinadamu, Juni 25, 2024 Jijini Dodoma. Afisa Mtendaji Mkuu na Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Bw. Frank K. Frank akitoa taarifa ya utangulizi kwenye Kikao Kazi cha kutathmini hali ya Utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano na kuzindua Taarifa ya kitakwimu ya usajili wa matukio muhimu ya kibinadamu, Juni 25, 2024 Jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA Dkt. Amina Msengwa akitoa salaam za Bodi hiyo kwenye Kikao Kazi cha kutathmini hali ya Utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano na kuzindua Taarifa ya kitakwimu ya usajili wa matukio muhimu ya kibinadamu, Juni 25, 2024 Jijini Dodoma. Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma Bw. Abdulrahman Mshamu akitoa

SHERIA ZA UANGALIZI WA UTAJIRI ASILI NA MALIASILIA ZA NCHI KUHUISHWA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya rasimu ya Mkakati wa mwaka 2024 – 2029 wa utekelezaji wa Sheria za Uangalizi wa utajiri asili na Maliasilia za nchi Sura 449 na 450. Juni 24, 2024 Ofisi za Bunge Dodoma. Mkurugenzi wa Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri Asili na Maliasilia za Nchi DCP Neema Mwanga (mwenye laptop), akitoa taarifa ya maandalizi ya rasimu ya Mkakati wa mwaka 2024 – 2029 wa utekelezaji wa Sheria za Uangalizi wa utajiri asili na Maliasilia za nchi Sura 449 na 450, tarehe 24 Juni, 2024 ofisi za Bunge Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea taarifa ya maandalizi ya rasimu ya Mkakati wa mwaka 2024 – 2029 wa utekelezaji wa Sheria za Uangalizi wa utajiri asili na Maliasilia za nchi Sura 449 na 450. Mkakati huo wenye lengo la kuhakikisha kuwa uvunaji na matumizi ya utajiri asili na Maliasilia za nchi unazingatia maslahi ya

JAMII IELIMISHWE JUU YA USULUHISHI NJE YA MAHAKAMA - JAJI MKUU

Image
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis  Juma akiongea wakati wa mazungumzo alipokutana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Jumanne Sagini Ofisi za Mahakama ya Rufani Kivukoni Jijini Dar es Salaam Juni 20, 2024. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Jumanne Sagini akiongea wakati wa mazungumzo alipokutana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma Ofisi za Mahakama ya Rufani Kivukoni Jijini Dar es Salaam Juni 20, 2024. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis  Juma akiongea wakati wa mazungumzo alipokutana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Jumanne Sagini Ofisi za Mahakama ya Rufani Kivukoni Jijini Dar es Salaam Juni 20, 2024. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima - WKS Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis  Juma amesema kuwa ni vyema Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ikaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida za kufanya usuluhishi wa migogoro nje ya Mahakama ili kuepuka kutumia muda

SIMAMIENI HAKI ZA BINADAMU – CP TENGA

Image
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini CP Nicodemus Menyamsumba Tenga akitoa hotuba ya utangulizi katika uzinduzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa Jeshi la Polisi na Magereza katika masuala ya huduma za msaada wa kisheria, Juni 12, 2024 jijini Arusha. Bi. Veronica Sigalla akimwakilisha Mkurugenzi Mkazi wa UNDP hapa nchini akitoa shukrani kwa Jeshi la Magereza na Polisi kwa ushirikiano katika kutekeleza masuala ya haki nchini, Juni 12, 2024 jijini Arusha. Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Ester Msambazi akielezea jinsi wizara ilivyojipanga katika kuhakikisha msaada wa kisheria unawafikia wananchi.  Juni 12, 2024 jijini Arusha. Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Candid Nasua akitoa moja ya mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa Jeshi la Polisi na Magereza katika masuala ya huduma za msaada wa kisheria,  Juni 12, 2024 jijini Arusha. Mgeni Rasmi na Meza Kuu wakiwa katika picha ya p

ORODHA YA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA NCHINI IANDALIWE -WAZIRI CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Msaada wa Kisheria kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (hayupo katika picha), Juni 10, 2024 Jijini Dodoma. Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kushoto), Naibu Waziri Mhe. Jumanne Sagini wakipokea taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Msaada wa Kisheria   kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (hayupo katika picha), Juni 10, 2024 Jijini Dodoma. Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (wa pili kushoto) kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi kwa Mhe. Waziri Pindi na Naibu Waziri Sagini, Juni 10, 2024 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Hyasinta Kissima-WKS  Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Dkt. Balozi Pindi

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA WATOTO – DKT. CHANA

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati anafungua Mdahalo kuhusu Sera za ajira kwa Watoto, Juni 05, 2024 Jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Washiriki kwenye Mdahalo kuhusu Sera za ajira kwa Watoto, Juni 05, 2024 Jijini Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxx Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 05, 2024 jijini Dar es Salaam amefungua mdahalo kuhusu Sera za ajira kwa watoto uliolenga kuimarisha  ulinzi wa watoto katika kuelekea kukomesha utumikishwaji  wa Watoto Tanzania. Akizungumza katika mdahalo huo Mhe. Chana amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia haki za watoto na hatua kali zitachukuliwa kwa wote wanaokiuka sheria inayomlinda mtoto. Chana ameongeza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kumlinda mtoto kwa nafasi yake. "Wajibu wetu kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha mtoto analindwa, Wazazi nyumbani, Viongozi wa Dini, Walimu mashuleni na jamii kwa ujumla tushirikiane na Serikali tuhakikishe mtoto analindwa." Alisema.

WANANCHI MAKETE WAIFAGILIA MSLAC

Image
  Rose Mbogela mkazi wa kijiji cha Matamba Kata ya Matamba akitoa kero yake kwenye mkutano wa kampeni ya MSLAC uliofanyika Juni 3, 2024 kijijini hapo. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx William Mabusi – WKS Makete Wananchi Wilayani Makete wamesema Kampeni ya Msaaada wa Kisheria ya Mama Samia imewapa elimu ya kutosha kuwaepusha na migororo, wakati huo huo imewasaidia pakubwa kutatua migogoro waliyokuwa nayo. Wananchi hao wametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa mikutano ya hadhara ya kutekeleza Kampeni hiyo Wilayani humo. Bw. Amos Tweve mkazi wa kijiji cha Nkenja Kata ya Kitulo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Juni 04, 2024 amesema “mtafikiri mlinusa kijiji hiki kina shida fulani mkaona mpeleke watu wenye taaluma hii waje kufundisha hiki mlichofundisha, naombeni elimu hii muifikishe kwa wantanzania wengine.” Katika mkutano huo Bw. Daudi Kinga alisema “nyie hamjui tu ila kwa elimu hii kuna migogoro mingi mmeitatua, Mungu awabariki sana, nawaomba wananchi wenzan

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YATAKIWA KUITUPIA JICHO SHERIA ZA USAFIRI WA ARDHINI

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro. Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo akiongea wakat wa kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati), wengine ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Winfrida Beatrice Korosso (kushoto) na Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo. Juni 03, 2024 Morogoro. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku & Bashiru Msangi - WKS Morogoro Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imetakiwa kuangalia upya sheria za usafiri ardhini kwa kuzifanyia mapitio na utafiti wa kina kwa kuw