ORODHA YA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA NCHINI IANDALIWE -WAZIRI CHANA

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Msaada wa Kisheria kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (hayupo katika picha), Juni 10, 2024 Jijini Dodoma.


Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kushoto), Naibu Waziri Mhe. Jumanne Sagini wakipokea taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Msaada wa Kisheria   kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (hayupo katika picha), Juni 10, 2024 Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi (wa pili kushoto) kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi kwa Mhe. Waziri Pindi na Naibu Waziri Sagini, Juni 10, 2024 Jijini Dodoma.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Hyasinta Kissima-WKS 

Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Dkt. Balozi Pindi Chana akiwa ameambata na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Jumanne Sagini ameagiza kuandaliwa kwa orodha "Directory" ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria Nchini, ili kuwawezesha Wananchi kuwatambua wakati wanapohitaji Msaada wa Kisheria. 

Waziri Chana ameyasema hayo tarehe 10 Juni, 2024, jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mafunzo  kwa Wasajili Wasaidizi wa Watoa Msaada wa Kisheria   kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi, mafunzo ambayo yaliyofanyika jijini Mbeya tarehe 6 -7 Juni, 2024 na kufunguliwa na Waziri mwenye dhamana. 

"Tunawapongeza Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria kwa kufanikisha  mafunzo hayo na  kuendelea kuwajengea uwezo Wasaidizi hao katika kuhakikisha Wizara inawafikia Wananchi katika maeneo mbalimbali na wanahudumiwa na Wataalamu wenye uelewa wa masuala mtambuka ya Kisheria. Jambo la muhimu nasisitiza tuandae orodha "Directory" ya Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria Nchini  ili tuweze kuwatambua katika kila Mkoa." Alisema Waziri Chana 

Ikumbukwe kuwa Lengo la uwepo  wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na Wataalamu wa Wizara ya Katiba na Sheria ni kusaidia kusikiliza na kushughulikia changamoto za Kisheria zilizopo kwenye maeneo yao hususani changamoto za masuala ya Ardhi, Wosia na Mirathi, Ndoa, Matunzo kwa Watoto na Migogoro mingineyo inayohitaji msaada wa Kisheria.



Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA