PINDI CHANA AFUNGUA MAFUNZO YA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA
Afisa Mtendaji Mkuu na
Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Bw. Frank K. Frank akitoa taarifa ya utangulizi
kwenye Kikao Kazi cha Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za
Usajili wa Matukio Muhimu ya Kibinadamu, Juni 27, 2024 Njombe.
Baadhi ya Washiriki kwenye Kikao
Kazi cha Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa
Matukio Muhimu ya Kibinadamu, Juni 27, 2024 Njombe.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na
Mwandishi Wetu - Njombe
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 27, 2024 amefungua mafunzo kwa Makatibu
Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na
Udhamini yaliofanyika katika ukumbi wa Agreement mkoani Njombe.
Mhe. Pindi Chana akifungua
mafunzo hayo amesisitiza juu ya umuhimu wa Usajili wa matukio muhimu ya
binadamu kama vizazi, vifo na sababu zake, ndoa na talaka kwani takwimu hizo
zinasaidia Serikali katika kupanga maendeleo.
“Tumekuwa tukizitumia
takwimu hizi katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na huduma kwa jamii, hivyo natoa
maelekezo kwa Ofisi zote za Mikoa ndani ya Tanzania Bara ziwe zinaandaa taarifa
za robo mwaka za usajili wa matukio muhimu ya Binadamu ambazo zitabainisha
Mafanikio na changamoto na kuziwasilisha RITA ili ziweze kufanyiwa kazi.”
Alisema.
Comments
Post a Comment