RAIS TLS AISHAURI WIZARA KUJIKITA KWENYE MAGEUZI YA HAKI JINAI

 

Mtaalam Mshauri wa mradi wa Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika Kupambana na Rushwa Nchini – BSAAT na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Harlod Sungusia akitoa mada ya utekelezaji wa Mradi wa BSAAT na Upimaji Matokeo ya Mradi huo. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

Kikao Kazi cha kufanya Tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24 na kuandaa Mpango Kazi wa mradi kwa mwaka 2024/25. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

Bw. Oswin Mkinga mmoja wa washiriki wa Kikao Kazi cha kufanya Tathmini ya mradi wa BSAAT kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24 na kuandaa Mpango Kazi wa mradi kwa mwaka 2024/25 akichangia hoja. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo akifafanua jambo kwenye Kikao Kazi cha kuandaa Andiko la Kuanzisha Mfuko wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

Sehemu ya washiriki kwenye Kikao Kazi cha kuandaa Andiko la Kuanzisha Mfuko wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

William Mabusi – WKS Morogoro

Mtaalam Mshauri wa mradi wa Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika Kupambana na Rushwa Nchini – BSAAT na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Harlod Sungusia ameishauri Wizara ya Katiba na Sheria kujikita kwenye mageuzi ya haki jinai ili kuwaongezea imani wananchi kwenye mifumo ya haki jinai na namna ya kushughulika na uhalifu wa kifedha.

Wakili Sungusia ameyasema hayo alipokuwa anatoa mada ya Utekelezaji wa Mradi wa BSAAT na Upimaji Matokeo ya Mradi huo na Mpango Kazi kwa mwaka 2024/25. Juni 29, 2024 mjini Morogoro.

 “Mradi wetu wa BSAAT unafika ukomo mwezi Machi, 2025. Nashauri baada ya ukomo wa BSAAT Wizara kujikita kwenye mageuzi ya haki jinai na namna ya kushughulika na uhalifu wa kifedha yaani utakatishaji fedha haramu na makosa tangulizi katika utakatishaji fedha haramu.” Alisema.

 Wizara ya Katiba na Sheria inaendesha Vikao Kazi viwili mkoani Morogoro; cha kwanza kikiwa na jukumu la kufanya tathmini ya mradi huo kwa kazi zilizofanywa mwaka 2023/24 na kuandaa Mpango Kazi wa mradi kwa mwaka 2024/25, Kikao Kazi cha pili kinaandaa Andiko la Kuanzisha Mfuko wa Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA