TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YATAKIWA KUITUPIA JICHO SHERIA ZA USAFIRI WA ARDHINI

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia wakati akifungua kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro.

Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo akiongea wakat wa kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati), wengine ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Winfrida Beatrice Korosso (kushoto) na Katibu Mtendaji Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. George Mandepo. Juni 03, 2024 Morogoro.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Juni 03, 2024 Morogoro.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lusajo Mwakabuku & Bashiru Msangi - WKS Morogoro

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imetakiwa kuangalia upya sheria za usafiri ardhini kwa kuzifanyia mapitio na utafiti wa kina kwa kuwa zimeonekana kutodhibiti kikamilifu ajali za barabarani ili ziweze kuwalazimisha wamiliki wa vyombo hivyo kuimarisha huduma na kuwapunguzia kazi madereva kwa kuendesha mwendo mrefu kama hatua za kupunguza ajali za barabarani.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 03/06/2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kikao kazi cha Kamisheni ya Tume hiyo ambacho kimefanyika Mkoani Morogoro katika hoteli ya Morena kwa ajili ya  kupitia taarifa saba (7) za utafiti uliofanywa hivi karibuni.

Waziri huyo ameonesha masikitiko yake jinsi ajali za barabarani hususan kwa mabasi yaendayo masafa marefu zinazotokana na makosa yanayoweza kuzuilika zinavyopoteza maisha ya wananchi na kuwasababishia ulemavu wa kudumu.

“Umefika wakati Tume ya Kurekebisha  Sheria Tanzania kufanya utafiti na kuja na mapendekezo madhubuti  yatakayosaidia kuondoa ajali za barabarani ili kulinda afya na maisha ya watanzania kwa kuwalazimisha wamiliki kuajiri dereva zaidi ya mmoja katika chombo kimoja cha masafa marefu” alisema Waziri.

Mhe. Chana ameagiza Tume  hiyo kushirikiana na  wasimamizi wa sheria ya barabarani  ili kutafuta suluhisho la kudumu la kuwalinda wasafiri  kwa usalama na kuhakikisha wanafika kwa wakati, huku akiligusia swala la bima za maisha katika kuwasidia waathirika.

“Sisi kama wabobevu wa sheria lazima tuangalie kama kampuni inapata ajali za mara kwa mara waachane na biashara ya kusafirisha watu na badala yake wasafirishe mizigo.” alisema

Aidha, ameendelea kueleza kwamba Tume ya Kurekebisha Sheria kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ambao ndio wenye dhamana hazipotayari kuona wananchi wakipoteza maisha kila kukicha.

Waziri Chana pia ameitaka Tume ya Kurekebisha Sheria wasisubiri kuletewa kazi za utafiti au mapitio  kama ilivyo sasa na badala yake wafanye kulingana na wanavyoona hali halisi na  wanayoyapata wakati wa utafiti.

Hata hivyo Mhe. Waziri aleeza kufarijika kwake na utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai yanayofanywa na Tume hiyo ambazo ni Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Nchini; Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha 91(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai;

Utekelezaji mwingi umekuwa katika Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na Watoa Taarifa;  Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana;  na  Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Adhabu ya Viboko Mahakamani na Katika Magereza.

Awali akimkaribisha Waziri huyo Jaji wa Mahakama ya Rufani, Winfrida Beatrice Korosso, ambaye ni  Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, alieleza kwamba Kikao cha Kamisheni ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Kikao cha 94 toka Tume hiyo kuanzishwa ambapo Tume, inatekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kuhakikisha vikao vyote vya Kisheria vinafanyika  hususan baada ya utafiti na mapitio ya kitaaluma.

Aidha, alieleza kwamba Taarifa zilizokamilishwa na Sekretariati ya Tume  baada ya kufanyika Mapitio, Utafiti na Tathmini  katika nyanja mbalimbali za sheria ni Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Nchini na Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Kifungu cha 91(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Kuhusu Uondoshaji wa Mashauri Mahakamani.

Pia taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Mashahidi na Watoa Taarifa; Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Usafiri Ardhini; Taarifa ya Mapito ya Mfumo wa Sheria Zinazosimamia Dhamana; Taarifa ya Mapitio ya Sheria Zinazosimamia Adhabu ya Viboko Mahakamani na Magereza;naTaarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria Zinazosimamia Hakimiliki na Hakishiriki.




Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA