NATAKA WATUMISHI WAWAJIBIKAJI – MASWI
Aliyekuwa Katibu Mkuu na sasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo akitoa neno la shukrani kwa Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi na Katibu Mkuu Eliakim Chacha Maswi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi, Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma.Aliyekuwa Katibu Mkuu na sasa
ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara
ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi nyaraka mbalimbali za Wizara
wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi, Julai 30, 2024 Mtumba
Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa
Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya Ofisi kati ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Mary Makondo na Katibu Mkuu mpya Bw.
Eliakim Chacha Maswi. Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na Sheria Eliakim Chacha Maswi akisalimiana na baadhi wa Watumishi wa
Wizara ya Katiba na Sheria wakati alipowasili kwa ajili ya hafla ya
makabidhiano ya ofisi. Julai 30, 2024 Mtumba Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
William
Mabusi na Hyasinta Kissima – WyKS Dodoma
Katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha Maswi amewataka watumishi wa
Wizara hiyo kuwajibika katika majukumu yao ili kutimiza malengo ya Wizara na
matarajio ya wananchi.
Bw. Maswi ameyasema
hayo kwenye hafla ya kukabidhiana ofisi kati yake na Bi. Mary Makondo
aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma, tarehe 30 Julai, 2024 ofisi za
Wizara Mtumba, hafla iliyohudhuriwa na watumishi na Menejimenti ya Wizara.
“Nawaomba mambo makubwa
mawili; kwanza, nahitaji utumishi uliotukuka, utumishi huo uambatane na
ushirikiano bila majungu wala makundi. Pili, nahitaji watumishi wawajibikaji.”
Alisema na kuongeza “Tumeomba kazi wenyewe na wengine tumetoka Ukuryani sasa
tufanye kazi.”
Akiongelea kuhusu
ushirikiano kati ya Menejimenti na watumishi wa chini yao amesema, “Watumishi
walio chini yako ndiyo wanaokufanya uwe boss hivyo tuwathamini na kuwasaidia.
Hawa wadogo ndiyo wanatufanya tuwe Viongozi, orodha ya malipo inayokuja kwangu
ianze na wadogo ili tuwasaidie na kuwatia moyo.”
Aidha, Bw. Maswi
amewataka Wakuu wa Idata na Vitengo kuwaacha watumishi walio chini yao
kuonyeshe uwezo wao, “kama sisi tusingepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wetu
tusingeaminiwa na leo kuwa hapa, tuwaache nao wajulikane kama hutaki mtu
aonekane wewe mwanga?”
Akiongea katika hafla
hiyo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake
wa kufanya mabadiliko ya uongozi kwa mujibu wa Katiba, “mabadiliko ambayo
ameyafanya Mhe. Rais tumeyapokea na tunawatakieni kila la heri kwenye majukumu
yenu mapya.” Amesema huku akimtaja Bw. Maswi kuwa ni kiongozi wa mabadiliko
chanya.
Mhe. Sagini amewasihi
watumishi wa Wizara kuendeleza umoja, “ameondoka Mary amekuja Maswi, nasaha
zangu kwenu nikitumia maneno ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya
Kikwete, nanukuu,"mimi Jakaya Kikwete nimemaliza muda wangu na sasa
anakuja Rais ambaye approach yake ya mambo inaweza kuwa tofauti.” mwisho wa
kunuu. Naomba mtambue Katibu Mkuu sasa ni Maswi, tujifunze kwa wapesi na
kufanya anavyotaka, tuache kulinganisha Mary na Maswi.
Aidha, Mhe. Sagini
amemshauri Katibu Mkuu huyo kuratibu vikao vya mara kwa mara na Wakuu wa
Taasisi za Wizara ili kuepusha vikao vya dharura kwa lengo la kuongeza
ushirikiano kati ya Taasisi za Wizara.
Akiongea katika hafla
hiyo Bi. Makondo amempongeza Katibu Mkuu mpya kwa kuteuliwa kuwatumikia
wananchi kupitia Wizara ya Katiba na Sheria. Wizara ambayo imepewa jukumu la
kusimamia masuala ya haki na sheria huku akiwataka watumishi
kumpa ushirikiano.
Comments
Post a Comment