SERIKALI YATOA MSIMAMO KUHUSU DHANA YA WATU ASILIA (INDIGENOUS PEOPLE)
Na
Lusajo Mwakabuku - WKS Geneva
Waziri wa Katiba na Sheria,
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana, amefanya mazungumzo na Mtaalam Maalum wa
Umoja wa Mataifa anayeangalia masuala ya Haki za Watu Asilia (Indigenous
People) Bwana Francisco Cali Tzay tarehe 3 Julai 2024.
Kupitia kikao hicho, Waziri
wa Katiba na Sheria, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
hapa Geneva Mhe. Balozi Dkt. Abdallah Possi na Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria
Bi. Mary Makondo wameeleza msimamo wa Serikali kutounga mkono dhana ya watu
asilia kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania.
Aidha, wamefafanua mafanikio
ya kisera, kisheria na kitaasisi ya kuhakikisha kila mtanzania anapata haki
zake za msingi bila kubaguliwa. Vilevile, walieleza jinsi suala la Ngorongoro
linavyoshughulikiwa kwa uwazi na kwa haki kwa kuwa wakazi katika hifadhi ya
Ngorongoro wanahama kwa hiari.
Waziri Chana alitumia nafasi
hiyo kumuahidi mtaalam huyo ushirikiano
kipindi atakapo kuja nchini kujionea mwenyewe hali halisi ya jinsi suala hili
linavyotekelezwa.
Kikao hiki ni sehemu ya
majadiliano yanayotokana na ushiriki wa Tanzania katika Kikao cha 56 cha Baraza
la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva - Switzerland katika ofisi za
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Comments
Post a Comment