TANZANIA IMEWEKA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UMASKINI – PINDI CHANA
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akichangia mjadala kwenye Kikao cha 56 cha Baraza
la Haki za Binadamu kinachoendelea katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa Geneva, Switzerland. Julai 2, 2024.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na
Lusajo Mwakabuku – WKS Geneva
Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Tanzania imeweka mikakati
mbalimbali katika kuhakikisha inaondoa wimbi la umaskini uliokithiri katika
jamii ambao hupelekea maskini kupata Haki za kibinadamu kwa kiasi kidogo au
kutozipata kabisa.
Waziri Chana amesema hayo leo tarehe 02/07/2024
alipokuwa akichangia mjadala unaohusu umaskini uliokithiri na jitihada za
kuutatua katika kikao cha 56 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea
katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Geneva, Switzerland.
Waziri Chana amesema Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inafuata msingi wa maendeleo unaozingatia haki za
binadamu, maisha bora, utulivu wa amani
na umoja, utawala bora, kuwa na jamii iliyoelimika na yenye uchumi imara wenye
ushindani ni baadhi ya sifa kuu za Dira
ya Maendeleo ya 2025.
“Pia tuko katika mchakato wa
kuendeleza DIRA yetu ya maendeleo ya 2050 ambayo ni mchakato shirikishi
unaowaleta pamoja Watendaji wa Serikali na Wasiokuwa wa Serikali ili
kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika ajenda ya maendeleo”. Aliongeza
Pindi Chana
Waziri Chana alihitimisha
mchango wake kwa kuelezea jinsi Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ilivyofanya Sensa ya Kitaifa ya Watu na Makazi mwaka
2022 ikiwa ni nyenzo ya kimkakati itakayotumika wakati wa kuandaa mpango wa maendeleo
wa DIRA 2050 unaolenga kukomesha umaskini na kukuza haki za binadamu kwa
kuzingatia Maendeleo Endelevu.
Comments
Post a Comment