TATHMINI YA UKARABATI JENGO LA USULUHISHI IKAMILIKE KWA WAKATI
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) akiteta
jambo na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walipotembelea
jengo linalotarajiwa kutumika kama Kituo cha Usuluhishi lililopo Temeke,
jijini Dar es Salaam. Julai 6, 2024.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini (kulia) pamoja
na baadhi ya Viongozi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakitembelea jengo
linalotarajiwa kutumika kama Kituo cha Usuluhishi lililopo Temeke, jijini
Dar es Salaam. Julai 6, 2024.
xxxxxxxxxxxxx
Hyasinta
Kissima – WKS Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Katiba
na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Julai 6, 2024 akiwa ameambatana na baadhi ya
Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wametembelea katika jengo
linalotarajiwa kutumika kuwa Kituo cha Usuluhishi kilichopo Temeke,
jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Sagini
ameelekeza kuharakishwa kwa kazi ya kufanyika kwa tathmini ya ukarabati
wa jengo hilo inayofanywa na TBA ili ukarabati ukamilike kwa wakati na jengo
hilo lianze kutumika.
Aidha, Mhe. Sagini ameelekeza
Sekretarieti ya Kituo cha Usuluhishi kianze kuandaliwa mapema ili jengo
litakapokuwa limekamilika lianze kufanya kazi mara moja.
Comments
Post a Comment