UKAGUZI UNAONGEZA THAMANI KATIKA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI - MAKONDO
Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Serikali Esnath Nicodem (wa kwanza kulia) akiwasilisha taarifa ya Kaguzi zitakazofanyika ambapo Kaguzi za hesabu za Serikali za Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2023/2024.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiongoza kikao kilichowahusisha Wakaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Timu ya Menejimenti ya Wizara kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma, Julai 15, 2024.
Hyasinta
Kissima- WyKS
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na Sheria Bi. Mary Makondo amesema kuwa kaguzi mbalimbali zinazofanywa na
Serikali katika Taasisi zake zimewezesha kuboresha utoaji huduma na
kuongeza thamani na ubora wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi
hizo kwa Wananchi wake.
Bi. Makondo ameyasema hayo
Julai 15, 2024 wakati wa kikao cha ufunguzi wa kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za
Serikali za Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2023/2024,
kilichowahusisha Wakaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na
Timu ya Menejimenti ya Wizara kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara
Mtumba, jijini Dodoma.
"Tunashukuru kwa kuweza
kutupitisha katika taarifa ya Kaguzi ambazo mnataraji kuzifanya kwa
kipindi mtakapokuwepo hapa kwani kupitia Kaguzi mnazozifanya tunapata mwongozo
wa namna bora ya kuwahudumia Wananchi. Wizara itawapatia ushirikiano wa kutosha
katika kukamilisha Kaguzi zenu ikienda sambamba na upatikanaji wa nyaraka
katika utekelezaji wa majukumu mahsusi.” Alisema Katibu Mkuu.
Comments
Post a Comment